PreGE2025 Mbunge Eric Shigongo aahidi Milioni 5 kwa ukarabati wa Kanisa Kome

PreGE2025 Mbunge Eric Shigongo aahidi Milioni 5 kwa ukarabati wa Kanisa Kome

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

upupu255

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
341
Reaction score
476
Mbunge wa Buchosha Mhe. Eric Shigongo ameahidi kutoa kiasi cha Tsh. Milioni 5 kwenye harambee ya Ukarabati wa jengo la kanisa Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima Kome iliyoandaliwa na Muhashamu Askofu Flaviani Katindi Kasala wa Jimbo Katoliki la Geita, kwa kushirikiana na Baba Paroko Padri Japheth Masalu wa Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima Kome.

Mhe. Shigongo ametoa ahadi hiyo kupitia mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Screenshot 2025-04-02 100010.png
 
Mwaka wa uchaguzi huu! Rostam ameahidi, Abdul ameahidi/ametoa, Injinia Hersi ameahidi milioni 5, Said Mtanda ameahidi milioni 5 kwenye huo ukarabaati.

Na mimi ngoja nijipange ili nije na ahadi yangu.
 
Back
Top Bottom