Mbunge CUF awashukia wenzake wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge CUF awashukia wenzake wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 12, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  JUMATANO, SEPTEMBA 12, 2012 05:19 NA BAKARI KIMWANGA, PANGANI

  MBUNGE wa Viti Maalumu, Amina Mwidau (CUF), amesema wingi wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umekuwa ni kikwazo kwa wabunge wa upinzani, kwa kuwa baadhi yao wana kazi ya kuzomea wenzao hata yanapojadiliwa masuala ya kitaifa.

  Kutokana na hatua hiyo, aliwataka wananchi kuhakikisha wanawakataa katika masanduku ya kura itakapofika mwaka 2015 na hatimaye Bunge hilo liwe na wabunge wengi kutoka vyama vya upinzani.

  Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana katika mkutano wa kijiji ambapo alikabidhi msaada wa pampu ya kusukumia maji kwa wananchi wa Kijiji cha Mwera.

  “Leo nchi imekuwa na matatizo kila kona kutokana na kusekana na wabunge wa kweli ambao wana uchungu wa kuwatetea wananchi na ninayasema haya mchana kweupe idadi ya wabunge wengi wa CCM imekuwa ni kikwazo kwetu sisi wapinzani.

  “Hata nanyi wananchi wa Mwera mnalitambua hilo, kutokana na hali hii na hata mbunge mwenzangu wa jimbo hilo ambaye anatokana na CCM hana muda wa kurudi tena tangu mlipomchangua. Kwa zaidi ya miaka miwili sasa hajarudi tena na hata leo hii mna tatizo la maji kwa mota kuungua hana habari nanyi.

  “Kuweza kupambana na mfumo huu mbovu ulioandaliwa na CCM kutokana na sera zake kuwa mbovu tunahitaji kujenga nchi kwa kuwa na viongozi majasiri kama Profesa Lipumba ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipigania haki za Watanzania.

  “Ninakabidhi mashine hii yenye thamani zaidi ya shilingi milioni tano kuweza kutatua kero ya maji katika kijiji hiki cha Mwera, ninajua uchungu wa maji kwa kuwa hali hii iliyopo sasa wanaopata tabu ni wanawake wenzangu na watoto ambao hutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kufanya shughuli za uzalishaji maji,” alisema Mwidau.

  Aidha, alionyesha wazi kukwama kwa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s) kutokana na Serikali kuwa na sera mbovu hasa katika kuwaongoza wananchi bila kujua matatizo yanayowakabili.

  “Huwezi kujenga shule bila walimu na hili linalotokea nchini kwetu katika shule zetu hizi za kata hakika ni kiini macho kikubwa, Serikali imejenga shule hizi huku vigogo wa ngazi za juu wakipishana katika kona za ndani na nje ya nchi kupeleka watoto wao katika shule binafsi ambazo Mtanzania wa kawaida hana uwezo wa kulipia ada.

  “Tunahitaji kuwa na mipango endelevu na kupitia CUF tumejipanga kuwa na jamii imara iliyostawi kwa kuiwezesha kwa kuipatia mahitaji muhimu ya kijamii sambamba na uwepo wa vifaa kama vya hospitali, shule na hata katika kuimarisha sekta ya maji na barabara,” alisema Mwidau.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwera, Hamisi Khalifan (CUF), alisema mashine hiyo ya kusukumia maji itakuwa ni mkombozi wa wananchi wake na vijiji vya jirani.

  “Sina hata la kusema maana hata macho yangu hayaamini kutokana na adha ya maji iliyopo hapa Mwera, ila ninapenda kukuhakikishia tutailinda na kuihifadhi mashine hii muhimu na mkombozi kwetu.

  “Nilileta maombi kwako nawe umeweza kuyatekeleza nami ninasema mbele ya mkutano huu mkubwa wa wana Mwera, sasa tumepata mkombozi wa kweli ambaye ni kimbilio la kweli na uhakika kwa wana Pangani.

  “Tutatunza vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira kwa kuhamasisha upandaji miti ya kisasa na inaweza kuwa ni chemichemi ya kuwa na vyanzo vingine vipya vya maji,” alisema Khalifan.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  No Comment...
   
 3. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 938
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Hivi cuf ni wapinzani au ccm b?mbona huyo mbunge wa cuf anawaponda washirika wao wa magamba?
   
 4. A

  Alhabaad Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
Loading...