YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,908
- 51,906
Dodoma. Mbunge wa Mtoni, Zanzibar (CCM), Abdulhafar Idrissa Juma ameshangazwa na kitendo cha Mfuko wa Maendeleo Nchini (Tasaf) kuziondoa kaya zinazomiliki vyoo vyenye masinki visiwani humo katika orodha ya wanufaika wa mfuko huo.
Juma amesema hayo jana Jumatano Aprili 7, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Amesema umasikini unatofautiana na mazingira hivyo ameeleza kuwa umasikini wa mtu wa Zanzibar hauwezi kufanana na masikini wa mtu wa Kigoma.
“Tasaf kama wanatafsiri kumiliki TV ya chogo Zanzibar ni kukosa sifa ya kuwa mnufaika, basi wanaweza kukuta wote hawafai kuwa katika Tasaf, lakini kumbe na wao ni watu masikini na wanastahili kusaidiwa na Tasaf” amesema.
Amesema kuwa katika jimbo lake kuna baadhi ya kaya zilizoondolewa katika orodha hiyo kwa sababu wanamiliki vyoo vyeme masinki, hivyo wamejipanga kukata rufaa.
Mbunge huyo ameitaka Tasaf katika kutekeleza majukumu yao kutofautisha vigezo vya umasikini kulingana na mazingira
Source: Gazeti la Mwananchi