barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,870
UKATILI WA KIJINSIA?
Mwanasiasa mkongwe Moses Wetang’ula Senator wa kaunti ya Bungoma, ambaye pia ni Waziri wa zamani wa mambo ya nje na Waziri wa zamani wa Biashara nchini Kenya. Jumapili ya tar.6 March (siku mbili kabla ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani) alipewa kipigo kikali na mke wake An Wacheke Ngugi hali iliyopelekea kukimbizwa hospitali kwa matibabu kabla hajaenda kuripoti Polisi ambapo alikuta mkewe ameshamtangulia kuripoti. Yani mke alimpiga mume kisha akawahi Polisi kusema amepigwa.
Hali hiyo ilipelekea kutengenezwa kwa picha hii na wapinzani wake kisiasa (photoshop) wakionesha alivyoathiriwa na kipigo cha mkewe. Licha ya kuwa picha hii ni photoshop lakini ni kweli kuwa Wetangula alipigwa na mkewe na kupatiwa matibabu ktk hospitali ya Bungoma.
Gazeti la Daily Nation la nchini Kenya limeripoti kuwa hii si mara ya kwanza kutokea mafarakano na kupigana kati ya Wetangula na mkewe Ann. Licha Ann kutoa kipigo hicho kwa mumewe lakini na yeye amekimbilia Polisi kumshtaki Wetangula. Kesi hii ni ya pili baada ya ile aliyofungua February 18 akidai kupigwa tena na mumewe.
Ann Wacheke Ngugi ni mfuasi wa muungano wa vyama vya siasa vya Jubilee Alliance vinavyoongoza serikali chini ya Rais Uhuru Kenyatta, licha ya kuwa mumewe ni kiongozi wa chama cha upinzani cha CORD. Tofauti ya kisiasa ya wenzi hao wawili inasemekana kuwa chanzo cha mfarakano ndani ya ndoa yao.
Kumekuwa na desturi kwa wanasiasa wengi nchini Kenya kupokea kipigo au kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na wake zao. Rais Kibaki na Arap Moi ni miongoni mwa viongozi wa juu wa nchi hiyo waliodaiwa kupigwa na wake zao. Wetangula pia ametangaza nia ya kugombea Urais mwakani. Ikiwa atapitishwa na chama chake na kushinda bila shaka ataendeleza list ya Marais wa Kenya kupigwa na wake zao. Je ingekua wewe ndo Wetangula ungefanyaje??
Kwa taarifa zaidi soma hapa Wetangula nursing injuries after being battered by wife - Nairobi News