Mbulu watakiwa kulima mazao ya biashara.

Mbulu watakiwa kulima mazao ya biashara.

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Wananchi Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, wametakiwa kulima mazao ya biashara ili kuondokana na umaskini.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mbulu Mhe.Chelestino Mofuga katika maadhimisho ya siku ya kilimo cha pareto iliyofanyika kijiji cha Muray katika Halmashauri ya mji wa Mbulu.

Kilimo hicho cha pareto ni maarufu Wilayani humo ambapo Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wananchi hao kuongeza mashamba ya zao hilo.

Amesema zao hilo ni pekee ambalo linavunwa kila baada ya wiki mbili ndani ya miaka mitatu kabla ya kubadilisha na kupanda upya na kukua hadi kuanza kuvunwa ndani ya miezi mitatu.

Akiwa katika maadhimisho hayo amewaagiza viongozi wote kuhakikisha kila mwananchi anajishughulisha na kilimo cha zao hilo ili kuendana na kasi ya kutokomeza umaskini nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu mjini bi. Anna Mbogo amesema zao hilo limewezesha Halmashauri kupata kipato pamoja na wakulima wa zao hilo kukarabati majengo ya shule ya msingi Muray kutokana na zao hilo kuwapatia kipato.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbulu mjini Bwana Vallerian Gidishan amewataka wakazi wa maeneo yanayolimwa pareto kutumia fursa hiyo vizuri kwani zao hilo linasoko la uhakika.

Akisoma taarifa ya kilimo cha zao hilo msimamizi wa kampuni ya TAICO inayojihusisha na kilimo hicho ndugu Gudlack Tairo amesema Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa pareto Duniani baada ya Australia ambapo mkoa wa Manyara ni mkoa wa tatu nchini kwa kuzalisha zao hilo.

Bwana Tairo amesema Halmashauri ya Mbulu mjini ilianza kulima zao hilo mwaka 2016 ambapo kilianza na vijiji vitatu ambavyo ni Muray,Hhayloto na Gwaami ambapo zilipatikana kilo gramu 9982 na mwaka 2018 vijiji viwili viliongezeka na kufikia vitano ambavyo ni Amoa na Maheri ambapo hadi kufikia mwezi march zilivunwa kilo gramu 24,337 za pareto.

MWISHO


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • IMG-20180819-WA0089.jpg
    IMG-20180819-WA0089.jpg
    97.6 KB · Views: 30
Back
Top Bottom