Mbuga ya MIKUMI

Mbuga ya MIKUMI

IDEGENDA

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
4,492
Reaction score
5,345
Katika kuorodheesha mbuga za wanyama Tanzania huwezi kuiacha mikumi. Lakini kitu kimoja huwa kinanishangaza katika mbuga hii, kila mwaka nikipita barabara ya Morogoro-Iringa hasa mwezi wa 10 huwa naona mbuga hii ikiwa imechomwa moto. Sasa naomba kuuliza nani huwa anachoma mbuga hii, na kwa nini, na Serikali huwa inakuwa wapi mpaka kitu muhimu kwa uchumi wa taifa kama mbuga inawaka moto???
 
Muulize katibu mkuu wa chama cha kijani ni mtumiaji mkubwa sana wa ile mbuga
 
Haichomwi kwa bahati mbaya, wanakusudia kabisa nia yaote majani mapya hata wavugaji huwa wanavanya hivi.
 
Exactly.
Yaani wanachoma yale manyasi "mazee" ili manyasi "machanga" yachipue ambayo ndio yana virutubisho zaidi.
 
Katika kuorodheesha mbuga za wanyama Tanzania huwezi kuiacha mikumi. Lakini kitu kimoja huwa kinanishangaza katika mbuga hii, kila mwaka nikipita barabara ya Morogoro-Iringa hasa mwezi wa 10 huwa naona mbuga hii ikiwa imechomwa moto. Sasa naomba kuuliza nani huwa anachoma mbuga hii, na kwa nini, na Serikali huwa inakuwa wapi mpaka kitu muhimu kwa uchumi wa taifa kama mbuga inawaka moto???

Hili ni swali zuri sana umeuliza. Katika uchomaji moto wa nyasi, kuna aina 2 ya uchomaji ambazo ni 1. Controlled fires. 2. Uncontrolled fires.
Na kwa swali lako hiyo ni controlled fire ambayo huwashwa na rangers aka mabwana pori. Moto huwashwa ili kutoa majani yaliokauka katika eneo husika ili kuipa ardhi nafasi yakutoa majani mapya yenye virutubisho kwa ajili ya wanyama pori. Na huwa moto huo umetengenezewa mipaka ambayo hauwezi kuvuka na kuunguza maeneo mengine ya pori ndo maana unaweza kuta zai ya ekari 50 zina waka moto au tayari zimechomwa na mahala pengine hapaja guswa.
 
Ndugu yangu Wolfpack nina wasiwasi na majiobu yako. Naona kama umeifanya issue ya kuchoma kuwa rahisi sana na kwamba ardhi inatayarishwa kwa ajili ya nyasi mpya. Tatizo langu ni kwamba, kwa nini sasa mbuga zote zisifanyiwe hivyo?
 
Back
Top Bottom