chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,400
- 24,982
Habari wanaBodi.
Awali ya yote nitangulie kwa kusema mimi ni mwanajimbo la HAI analoliongoza Mh Mbowe na mimi ni mmoja kati ya watu niliompigia kura ya NDIYO Mh Mbowe pamoja na kushawishi wengine pia kumchagua Bw Mbowe na hatimaye kuweza kuibuka na ushindi wa kishindo katika Jimbo letu.
Lengo la kuanzisha UZI huu ni moja tu nalo ni kumuhimiza Mhe Mbowe awakumbuke waliompa ridhaa ya kurejea tena bungeni kuwajilisha wanajimbo la HAI.
Wilaya ya HAI ni moja katika ya wilaya chache nchini zilizobahatika kupata maendeleo ya haraka toka kipindi cha Ukoloni lakini tunapoelekea sasa ni kwamba tunarudi nyuma zaidi hata ya kipindi cha Ukoloni kwani zamani umeme ulikuwa wa uhakika, maji ya uhakika, huduma za bora za afya, barabara bora za lami n.k
Maajabu ya sasa ni kwamba HAI imekuwa kama haina muwakilishi, siyo mbunge wala diwani kwani ni takriban miezi sita sasa watu wa HAI wanalala gizani kutokana na mgao mkali wa umeme usiokuwa na maelezo yoyote, shughuli za kimaendeleo zimekwama watu wanashinda vijiweni kutokana na ukosefu wa huduma ya msingi ya umeme, huduma za afya nazo zimedorora hakuna mwananchi ambaye anaridhika na huduma zinazotolewa katika zahanati za vijiji kwani hata dawa za kutuliza maumivu imekuwa tatizo.
Suala la MAJI nalo limekuwa utata, gharama za kuunganishiwa maji zimepanda kwa asilimia 50 na wakati vyanzo vya maji vyote vipo katika makazi ya watu iweje gharama za maji ziwe juu zaidi ya watu wa mjini?
Kero zote hizo siyo Mbunge Mhe Mbowe ama diwani ameshawahi kutolea ufafanuzi au wao wakishapewa kura tukae kimya tusihoji chochote?
Mhe Mbowe hama Dar es salaam rudi jimboni kwako ukatatue kero za wananchi wako waliokupa kura.
Tunataka kuona tofauti kati ya CCM na UKAWA/CHADEMA la sivyo hakuna sababu ya kuchagua tena wapinzani uchaguzi mkuu ujao, mbunge aliyekuwepo kipindi cha nyuma kupitia CCM alionekana kuwa karibu sana na watu wake, Mhe Mbowe ulipaswa kuiga hili siyo kuzunguka nchi nzima majukwaani huku watu wa jimboni mwako wakitaabika.
Wananchi wa HAI wana msimamo ndiyo maana wakachagua mabadiliko lakini hawajayaona mpaka sasa, CHADEMA itambue raia wakiamua kukabidhi jimbo kwa wana CCM basi CHADEMA itazikwa rasmi wilayani HAI maana hatutaki maigizo.
Mhe Mbowe usilewe madaraka na siyo kwamba wananchi ni wajinga watashindwa kukupiga chini mwaka 2020.
Kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya HAI tunaomba hizi kero zitatuliwe kwa wakati Mhe Mbowe ukishirikiana na madiwani wako!
Naomba kuwasilisha.......