Mbowe na TANROADS, mita 30 kutoka barabara ya Machame mna maana gani?

Habari wakuu,.

Kumekuwa na sintofahamu kubwa sana kwa wakazi wa wilaya ya HAI ambayo mbunge mwenye dhamana ni Mhe Freeman mbowe.

Hususan kwa wananchi ambao wapo karibu na barabara hii ya machame.

Kabla barabara hii haijakabidhiwa Tanroads ilikuwa chini ya serikali za vijiji na halmashauri ya wilaya ya HAI, sasa baada ya Tanroads kuichukua wakaanza kuweka "X " katika majengo yaliyopo mita 22.5 kutoka katikati ya barabara hii ya machame miaka mitano iliyopita bila kuahidi fidia yoyote na wala hakuna maelezo yoyote kutoka ofisi yoyote akiwemo mbunge wa Jimbo hili la wilaya ya HAI Mhe Freeman.

Sasa leo wamekuja kuweka "X " mpya lakini wamezidisha vipimo, kutoka mita 22.5 za awali kufikia mita 30 kwa sasa bila kulipa fidia yoyote zaidi ya kuandika BOMOA.

Kinachosikitisha wananchi wengi ni kwamba barabara hii haina matumizi makubwa kiasi cha kusababishia watu wakae mita 30.

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba hii barabara haipanuliwi bali wanataka wananchi wakae mbali na barabara.

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba hata barabara za miji mikubwa wananchi hawakai mbali na barabara kwa umbali huo.

Kinachosikitisha zaidi hata mbunge mwenye dhamana Mhe Mbowe amekaa kimya juu ya sintofahamu hii waliyonayo wananchi wake.

Kinachosikitisha zaidi inasemekana watalii hawapendi kuona nyumba zikiwa karibu na barabara, wanapenda kuona miti, vichaka, n.k Je tumefikia hatua hii ya kukosa uhuru tukiwa kwetu?

Kinachoaikitisha zaidi ardhi maeneo haya ni adimu sana na nyingi ni za urithi hivyo watu wanafukuzwa kwao.

Kinachosikitisha zaidi mwezi ujao wamesema wanaanza kubomoa nyumba za watu na notisi tiyari wameshatoa.

Wakuu niishie hapa maana inaumiza sana.
Kwahiyo ile ghorofa ya Ment pale Nfony inabomolewa? Hotel ya mdogo wake Mengi kule park je? Ile hotel pale Kyalia? Ile Petrol Station ya Machame pale Nfon? Kanisa la Urara?? Nyumba zote nzuri kando ya barabara zinabomolewa? This is sad..
 
Mkuu yote inafagiliwa, njoo mpaka posta, pandisha machame cotc, ngazi za kanisa la Nkwarungo, pia Nkwamwasi hawabakizi kitu, kyalia ndiyo maumivu kabisa, kule juu park wengi wapo karibu na barabara hivyo watalia sana, Kwa Mengi sina hakika,.

Hotel ya Mengi nayo tiyari imeshafunguliwa rasmi. Nimeona bango lao pale stand ya Machame hospital

Jamaa wana escort ya mtutu wa bunduki, naskia huko mfoni jamaa wa kuweka "X " walifanyiwa fujo kidogo wakatwe mapanga
 
Serikali ya kijiji haina info zozote mkuu, siyo mara ya kwanza kuulizia huko.

Machame sehemu gani mkuu, nazungumzia wahanga ambao ni wale waliojenga karibu na barabara mkuu
Barabara unayoizungumzia ni hii ya kupanda huko macheme juu au
 
Kwahiyo ile ghorofa ya Ment pale Nfony inabomolewa? Hotel ya mdogo wake Mengi kule park je? Ile hotel pale Kyalia? Ile Petrol Station ya Machame pale Nfon? Kanisa la Urara?? Nyumba zote nzuri kando ya barabara zinabomolewa? This is sad..
Na hizi nyumba zina zipendezesha Machame
 
Kinachonisikitisha ni watu kutokujua maana na umuhimu wa hifadh ya barabara

Kinachonisikitisha ni watu kufikiria leo tu bila kuwaza miaka mingi ijayo (makosa yaleyale yaliyofanywa na mipango miji dar enz hzo) kwa kuona barabara hazna matumz makubwa leo.

Kinacho nisikitisha zaid ni watu kutojua umuhimu wa serikal kubomoa na kuzuia uwekezaj zaid katka hifadh ili kupunguza hasara zaid

Kitakacho nifurahsha ni endapo sheria zitafwatwa na wanaostaili walipwe
 
Kinachokisikitisha zaidi na kuumiza roho, wamachame ni mashemeji zangu, nimeoa kwenu
 
Kwa uelewa wangu mita 30 kutoka bara barani ni mpango mpya na mabadiliko ya Tanroads kabla ilikua 22.5. na kwa sasa imeongezwa hadi mita 30 na kwa miji mikubwa mzee tambua kwamba zile bara bara za kwenye miji,manispaa au halmashaur ziko chini ya manispaa,jiji,halmashauri wanaohusika pale ni maafisa mipango miji pia wanataratb zao uwezi weka mijini mita 30 toka barabaran watapanga waokuftana na mji ulivykaa kama ni afisa mipango miji wa jiji ,manispaa au halmashaur ila kwa barabara kuu ambz ziko chini ya Tanroad utaratib wao kwa sasa ni mita 30 ndio maana wanafanya upanuzi
 
Barabara hii ni nyembamba sana, inahitaji ipate upana ea kutosha. Mtoa mada anafikiria mambo ya Leo tu. Miaka kumi ijayo itakuwaje? Kubomoa halikwepeki kwa maendeleo ya Machame.
 
Mkuu yote inafagiliwa, njoo mpaka posta, pandisha machame cotc, ngazi za kanisa la Nkwarungo, pia Nkwamwasi hawabakizi kitu, kyalia ndiyo maumivu kabisa, kule juu park wengi wapo karibu na barabara hivyo watalia sana, Kwa Mengi sina hakika,.

Hotel ya Mengi nayo tiyari imeshafunguliwa rasmi. Nimeona bango lao pale stand ya Machame hospital

Jamaa wana escort ya mtutu wa bunduki, naskia huko mfoni jamaa wa kuweka "X " walifanyiwa fujo kidogo wakatwe mapanga
Na pale Mfoni walivyo na fujo sidhani kama wanaweza kubomoa hivi hivi.. Hata wakienda hao askari na bunduki zao lazima damu itamwagika pale..

Daaah angalau hiyo Hotel ifungulie December nikirudi mapumzikoni nishinde hapo..
 
Mimi niko Dar, lakini tuna eneo letu hapo, mwaka jana nilikuta x kweli, lakini wakasema itachukua muda sana kuvunja na watu watalipwa fidia

Sasa hii habari ya kuvunja nyumba mwezi huu tena bila fidia yoyote, wakati barabara hiyo imekuta watu hapo na sio watu wamefuata barabara hiyo maana maeneo mengi hapo ni ya urithi sio ya kununua,

Huyo Mbowe naona kajisahau kama ni mbunge wa HAI mpaka wananchi waandamanaji ndio atakumbuka,

Cha msingi kifanyike kikao cha wananchi wa hapo na kutoka na uamuzi mmoja katika kudai haki yao, tuache kuwategemea Hawa wanasiasa uchwara ambao wako kimaslahi zaidi,

Inauma sana aisee!
Una maana gani kusema "ardhi ni urithi si ya kununua"? Hujui hata ardhi unayonunua ilirithiwa kutoka watu wengine ndipo warithi wakaiuza.
 
Ukitaka kujua uwezo wa watu wa kufikiri angalia coment zao.Tz kuna vichaa wengi wanaojiona wazima ndomana tuna buruzwa hata kwenye mambo ya msingi
 
Mimi niko Dar, lakini tuna eneo letu hapo, mwaka jana nilikuta x kweli, lakini wakasema itachukua muda sana kuvunja na watu watalipwa fidia

Sasa hii habari ya kuvunja nyumba mwezi huu tena bila fidia yoyote, wakati barabara hiyo imekuta watu hapo na sio watu wamefuata barabara hiyo maana maeneo mengi hapo ni ya urithi sio ya kununua,

Huyo Mbowe naona kajisahau kama ni mbunge wa HAI mpaka wananchi waandamanaji ndio atakumbuka,

Cha msingi kifanyike kikao cha wananchi wa hapo na kutoka na uamuzi mmoja katika kudai haki yao, tuache kuwategemea Hawa wanasiasa uchwara ambao wako kimaslahi zaidi,

Inauma sana aisee!

yuko lindi anakagua uhai wa chama
 
Katika maswala ya maendeleo yoyote katika maeneo husika lazma wananchi washirikishwe ndivyo sheria inavyo sema sio kila jambo linalo fanywa na serikali lipo sawa kunawakati wanavunja sheria kwa makusudi tu katika kutoa michango humu lazma ujue wananchi walishirikishwa?
 
Back
Top Bottom