Mbowe: Mbunge mmoja wa Chadema sawa na 30 wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe: Mbunge mmoja wa Chadema sawa na 30 wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 13, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe  Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema mbunge mmoja wa chama chake ni sawa na wabunge 30 wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM).

  Alisema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Chadema iliyofanyika juzi Usa River, wilayani Arumeru.
  Katika uzinduzi huo, Chadema kilikuwa kina mnadi mgombea wake Joshua Nassari anayewania kuwa mbunge wa Jimbo

  la Arumeru Mashariki kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Jeremia Sumari aliyefariki dunia hivi karibuni.
  “Ninaomba wananchi wa Arumeru, mnipatie Nassari kuwa mbunge , nadhani mmeona kazi za wabunge wa Chadema

  wakiwa bungeni, akisimama kutoa hoja utawaona wale wa chama cha magamba wanavyopata shida…mbunge mmoja wa Chadema ni sawa na wabunge 30 wa chama cha magamba,” alisema huku akishangiliwa.

  Alisema wabunge wa Chadema pamoja na uchache wao bungeni, lakini wamekuwa wakiwameza wabunge wa chama tawala wapatao 257.

  “Alisema endapo Nassari ataingia bungeni, atakuwa ameiongezea nguvu Chadema kwa uwingi wabunge ambapo nguvu yake itakuwa sawa na wabunge magamba wa CCM 30,” alisema na kuongeza kuwa endapo mgombea wake

  atachaguliwa chama chake kitakuwa na uwakilishi wa wabunge 49 bungeni.
  Mbowe alisema wabunge wa chama chake ni machachari na wamekwenda bungeni kufanya kazi moja tu ya kutetea maslahi ya Watanzania.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,811
  Likes Received: 17,911
  Trophy Points: 280
  ''Chagueni mtu ambaye atasikilizwa na Serikali na mtakayeshirikiana naye kutatua matatizo na sio mtu ambaye anasema kwa ukali ambaye anapotosha jamii." haya ni maneno ya mbunge wa CCM Mwigulu,akimaanisha kuwa CDM huwa hawasikilizwi na serikali, sasa huyu ni ukucha tu Tundu Lissu ambao ukirefuka kidogo unakatwa
   
 3. sheiza

  sheiza JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 1,786
  Trophy Points: 280
  ccm =wengi kwa namba ila wachache kwa uelewa,ujenzi wa hoja na mzigo kwa walipa kodi.

  cdm = wachache kwa namba ila wengi kwa uelewa,ujenzi wa hoja na kielelezo cha taifa.
   
 4. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 940
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Mheshimiwa Mbowe umesema kweli,wabunge wa Magamba si lolote si chochote kazi yao ni kusinzia,kupiga makofi na kuzomea ila kazi ya wabunge wa CHADEMA ni kutetea wanyonge.
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  CCM ni janga kwa Taifa letu kwa majira haya!

  Mageuzi ni sasa!
   
 6. Chali wa Moshi

  Chali wa Moshi JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  uwo niukweli usiopingika. nyie amuwaonaga jinsi wanavyo lala tuu na kusubiri waambie NDIO AU SIO.

  CCM ni janga la kitaifa.
   
 7. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kama ni kweli MBUNGE 1 CDM = WABUNGE 30 wa CCM. Tunaomba MDAHALO LIVE kati ya Nassari V Sioyi kabla ya April fool! WARNING hakuna kuingia mitini kwa kisingizio chochote kile.
   
 8. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Bange Mbaya! hivi Kwa nini viongozi wengi wa CDM wanapenda hii kitu?
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hakuna kitu hapa ngoja nipite tu!
   
Loading...