Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kesho tarehe 9/6/2013 anatarajiwa kuunguruma jijini Mbeya.
Kiongozi huyo wa upinzani bungeni anatarajiwa kutumia nafasi hiyo kumnadi mgombea udiwani wa CHADEMA kata ya Iyela Charles Nkelwa.
Mwenyekiti Mbowe anatarajiwa pia kuwatoa hofu wananchi wa kata ya Iyela kutokana na madai ya kuanzishwa makundi ya kiharamia jijini Mbeya yanayoratibiwa na mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba yenye lengo la kuwatisha wananchi wasijitokeze kupiga kura.
Mbeya ni ngome kuu ya CHADEMA kwa ukanda wa nyanda za juu kusini na ushindi wa chama hicho katika kata ya Iyela unatarajiwa kuwa wa kishindo.