Mbowe kisiki cha mpingo CHADEMA?

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,896
6,912
*MBOWE KISIKI CHADEMA*

*Chadema* ilianza kuja juu zaidi baada ya Slaa kujiunga. Slaa alipogombea Urais Chadema ikafikia kimo cha kuwa CHAMA KIKUU CHA UPINZANI.

Kukua na kuimarika kwa Chadema hakuwezi kulinganishwa na NCCR Mageuzi ya Mrema wakati ile, maana NCCR haikufurukuta majaribu hatimaye Mrema kutimkia TLP ya Magomeni Mapipa.

CUF pekee imeweza kistahimili majaribu kadhaa nchini ya uongozi thabiti wa Katibu Mkuu wake Maalim Seif.

Wengi walifikiri Slaa ndio nguzo ya Chadema kumbe sivyo. Alipopata jaribio la kukaribishwa Lowasa Slaa akabadilika ghafla hadi kwenda kumnadi mgombea CCM kisha kuishia kukimbilia Canada.

MBOWE kumbe ndio ni kisiki cha mpingo Chadema. Hashawishiki kwa kitu kidogo au kikubwa ili kusaliti Chama.

Je, jeuri ya Mbowe ni uwezo kifedha alio naona au utashi wa Mageuzi Tanzania?

Njia pekee ya kuking'oa hiki kisiki cha mpingo Chadema ni kumfilisi? Maana anajitolea bila malipo na ni mwenyekiti wa chama cha siasa pekee barani Afrika asiyelipwa mshahara kama mwenyekiti.
 
Ni kisiki kweli kweli wa kuuza chama na kusafisha mafisadi wa ccm.

2020 atamuuzia tena Lugumi na Bavicha wote mtalazimika kumsafisha.
 
Mbowe, tafadhali toa namba yako ya Account ali wanachama na wanothamini mchango wako kwa taifa hili wakulipe mshahara; mwenye mia, mia mbili, mia tano, buku, yote sawa. Umeandamwa saaaana, na wanye kutambua ugumu wa kazi yako wanakusikitikia lakini hawana jinsi ya kukusaidia. Lakini kama wapenda mabadiliko wakiamua kukulipa mfano hata miatano kila mwezi, waweza kulipa bill ya maji, mafuta ya gari, kodi kadhaa, airtime.

Nina uhakika wakiisha jiahakikishia wamekudhoofisha ki-biashara, kinachofuata ni kufunga ruzuku. Ruzuku haiwezi kufika 2020 kabla haijafutwa. Hii ya kumpa Lipumba ruzuku ni njia ya kuonyesha kuwa kodi ya serikali inalipa watu katika vyama ambao huzitumia kwa maslahi yao hivyo zoezi zima la ruzuku limesimamishwa.
 
Serikali ingekuwa inafanya kazi zake kwa kasi kama inavyowafatilia wapinzani na hasa Mbowe tungekuwa mbali.

Hivi kwa mfano NHC, kuanzia wamtoe Mbowe mbona hatuwasikii wakifanya kwa wateja wengine!!??

Au ndio kazi kwa maelekezo maalum??!
 
*MBOWE KISIKI CHADEMA*

*Chadema* ilianza kuja juu zaidi baada ya Slaa kujiunga. Slaa alipogombea Urais Chadema ikafikia kimo cha kuwa CHAMA KIKUU CHA UPINZANI.

Kukua na kuimarika kwa Chadema hakuwezi kulinganishwa na NCCR Mageuzi ya Mrema wakati ile, maana NCCR haikufurukuta majaribu hatimaye Mrema kutimkia TLP ya Magomeni Mapipa.

CUF pekee imeweza kistahimili majaribu kadhaa nchini ya uongozi thabiti wa Katibu Mkuu wake Maalim Seif.

Wengi walifikiri Slaa ndio nguzo ya Chadema kumbe sivyo. Alipopata jaribio la kukaribishwa Lowasa Slaa akabadilika ghafla hadi kwenda kumnadi mgombea CCM kisha kuishia kukimbilia Canada.

MBOWE kumbe ndio ni kisiki cha mpingo Chadema. Hashawishiki kwa kitu kidogo au kikubwa ili kusaliti Chama.

Je, jeuri ya Mbowe ni uwezo kifedha alio naona au utashi wa Mageuzi Tanzania?

Njia pekee ya kuking'oa hiki kisiki cha mpingo Chadema ni kumfilisi? Maana anajitolea bila malipo na ni mwenyekiti wa chama cha siasa pekee barani Afrika asiyelipwa mshahara kama mwenyekiti.
Wakati watu wamemnunua kwa bei poa, acha hizo, mtu akija ghafla hapa nchini asiulize lolote akaangalia mwenendo wa CHADEMA, alafu baadaye muulize mwenyekiti nani kati ya mbowe na Lowasa , atakwambia Lowasa
 
Kama Mbowe rahisi kununuliwa CCM wasingeingia gharama kubwa za kuwatumia akina Zitto Kabwe
 
Back
Top Bottom