MBOWE: Kilimanjaro hatutegemei CCM

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amefunguka na kusema kuwa mkoa wa Kilimanjaro hawategemei CCM kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo na kusema kitu pekee ambacho kinafanya mkoa huo kuwa wa mfano kwa mageuzi ni kutokana na elimu.


Mbowe.jpg

Freeman Mbowe amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Machame Uroki katika ziara yake ya jimbo na kusema kuwa Kilimanjaro inakuwa kimaendeleo kutokana na baadhi ya wazee miaka hiyo kupata elimu ya kutosha ambayo ndiyo imekuwa chachu ya maendeleo hayo.

"Sifa kubwa ya kwanza katika taifa hili kuhusu mkoa wa Kilimanjaro ni elimu, wazee wetu walisoma siyo wote ila wachache waliosoma walisoma sana kulinganisha na mikoa mingine kwa hiyo maendeleo ya Kilimanjaro hayategemei CCM, bala maendeleo ya Kilimanjaro yalikuwepo hata kabla ya uhuru watu walisoma siku nyingi na watu walipata imani siku nyingi, sifa hii ni lazima tuirejeshe, tuna shule nyingi lakini shule nyingi ni zile ambazo hazina sifa ya kuitwa shule" alisema Mbowe

Aidha Mbowe aliwataka watu kuwekeza nguvu kubwa kwenye elimu kwa watoto wao kutokana na ukweli kwamba ardhi ya kuweza kuwarishisha watoto kwa sasa haipo Kilimanjaro hivyo wanapaswa kuwekeza zaidi na zaidi kwenye elimu na kusema anatambua kuwa wanafanya hivyo ila bado haitoshi wanapaswa kuongeza nguvu zaidi na zaidi.
 
Yote yaliyopo kilimanjaro,ni matunda ya ccm,chini ya nyerere,mkapa so anaposema maendeleo anayasimamia yp?nmezaliwa ar chuga nimekulia moshi,toka nmekuja mosh nikiwa na 5yrs kil kitu kipo mpk kijijin kuanzia lami na umeme na mshule kibao,ss ukisema hatutegemei ccm wakat wao ndio waratib wa kila kitu nakushangaaa,

Niwapongeze mawaziri wa awam zilizopita kutoka mkoa wa kilimanjaro maana walipigana kuiwek kilimanjaro salama kwa barabara na nishati mpk kijin
 
Hata leo maendeleo ya mtu yoyote hayataletwa na CCM. Zimepita awamu 5 za uongozi chini ya CCM na ahadi kemkem za maendeleo na maisha bora, tumebaki kuvalishwa mavazi yenye sura za watu!

Cha muhimu PAMBANA NA HALI YAKO UKIMTANGULIZA MUNGU MBELE.
 
Kusema ukweli sipendi kabisa matamshi yanayohusisha na maeneo...

Kanchi Ketu bado kachanga Sana..... Kilimanjaro yenyewe haijapata Maendeleo ya kutosha bado.... Tuna haja ya kufikiria taifa letu Kwa ujumla wake Kwa kuwa kila mtanzania ana haki ya Kuishi popote anapotaka.....

Singida pasipokuwa na Maendeleo ni hasara Kwa kila mmoja wetu, vilevile Geita,Mara,Bukoba Au hata Kigoma.....

Mbowe fikiria taifa zima kwa sasa...... Achana na politics za kijieneo kidogo kwenye linchi maskini Kama letu
 
Back
Top Bottom