Mbowe aweka masharti umoja mpya na Zitto

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
24,150
Reaction score
56,463
FB_IMG_1527924281144.jpg

Kwa kifupi.

MH. Mbowe amesema umoja huo unakusudiwa kuongeza changamoto na nguvu mpya ya kisiasa nchini, lakini kuna haja ya kuangalia vyama unavyoungana navyo

"Umoja ni jambo jema utapunguza utani kwenye mambo serious ya kuendesha siasa ndani ya vyama, nasema utapunguza utani kwa sababu kuna vyama vina miaka 20 na zaidi lkn havina hata mkiti wa mtaa, sasa utaunganaje na chama kama hicho, ila kuna vingine vina muda mfupi lkn unaweza kuona vimefanya kitu". alisema Mbowe.

"Ila kwanza sijui kwa nini Zitto alizungumzia muungano wa vyama au umoja wa kidemokrasia msibani. Tulichokuwa tunafanya pale kwa kuwa mbunge alichaguliwa na wananchi wote ni kushirikiana kumhifadhi na baadaye kutafuta mgombea mmoja atakayekuwa na nguvu, lakini hilo suala sio la mimi kusema tu ni la vikao vya chama".
 
sasa hapo na wewe umetoa habari gani sasa au?
 
Ujinga ni kutuwekea kichwa cha habari badala ya habari yenyewe.
 
Mtoa mada anaandika akitokea Lumbumba kuchukua posho akiwa kwenye bajaji mitaa ya kariakoo na Msimbazi kuelekea kigogo kintiku kwao
 
Siku hizi posho hakuna chakubanga kadhibiti huoni hata team lumumba ilivyopungua humu.
 
Ila ujinga zaidi ni pale unaposubiri mtu mwingine akanunue gazeti akuandikie ili usome.

Hata hivyo usijali sana kasome tena post ya kwanza.
Bora umejiongeza...usifikiri wote tupo yanayopatikana hayo magazeti.!
 
"Ila kwanza sijui kwa nini Zitto alizungumzia muungano wa vyama au umoja wa kidemokrasia msibani. Tulichokuwa tunafanya pale kwa kuwa mbunge alichaguliwa na wananchi wote ni kushirikiana kumhifadhi na baadaye kutafuta mgombea mmoja atakayekuwa na nguvu, lakini hilo suala sio la mimi kusema tu ni la vikao vya chama
Zitto akili imemruka sasa Muda mwingi ni kama mtu anayeota
 
Bora umejiongeza...usifikiri wote tupo yanayopatikana hayo magazeti.!
Mbona hata kwenye web yao habari hii ipo au unataka na link nikutafutie hahaa watanzania kwa uvivu mnapenda raha sana.
 
Mbowe keshanusa..huyu zito si alishawahi wapitia wote akiwemo mzee wa bahari motors..ila mbowe akagoma..leo kaona anahitaji jimbo lirudi chadema ndiyo anajifanya kuondoa tofauti ili zitto awsaidie kurudisha jimbo..kisha umeona wapi watu wanaelewana jukwaani badala ya kukaa kwanza faragha watatue tofauti zao..kweli hizi ni nyakati za mfa maji kwa upinzani
 
Kwa mawazo yako unafikiri kati ya Mbowe na Zitto nani anamhitaji mwenzake zaidi.
 
View attachment 792003

Kwa kifupi.

MH. Mbowe amesema umoja huo unakusudiwa kuongeza changamoto na nguvu mpya ya kisiasa nchini, lakini kuna haja ya kuangalia vyama unavyoungana navyo

"Umoja ni jambo jema utapunguza utani kwenye mambo serious ya kuendesha siasa ndani ya vyama, nasema utapunguza utani kwa sababu kuna vyama vina miaka 20 na zaidi lkn havina hata mkiti wa mtaa, sasa utaunganaje na chama kama hicho, ila kuna vingine vina muda mfupi lkn unaweza kuona vimefanya kitu". alisema Mbowe.

"Ila kwanza sijui kwa nini Zitto alizungumzia muungano wa vyama au umoja wa kidemokrasia msibani. Tulichokuwa tunafanya pale kwa kuwa mbunge alichaguliwa na wananchi wote ni kushirikiana kumhifadhi na baadaye kutafuta mgombea mmoja atakayekuwa na nguvu, lakini hilo suala sio la mimi kusema tu ni la vikao vya chama".
Makubaliano ya Kakonko: Mbowe na Zitto walisema nini

Zitto mwenyewe huyo hapo... ameandikaaaa
 
Kwa mawazo yako unafikiri kati ya Mbowe na Zitto nani anamhitaji mwenzake zaidi.
Kwa kigoma huko ambako chadema imepoteza mbunge na wanataka kurudisha kiti chao bungeni mbowe anamuhitaji zitto kwa sasa kuliko mwanachama au mbunge yeyote wa chadema.
 
Back
Top Bottom