Mbowe aunguruma Ukerewe leo Ijumaa 13/1/2017

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,Mhe. Freeman Mbowe leo Ijumaa 13/1/2017 amewasili kwa Pantoni katika jimbo la Ukerewe jijini Mwanza na kupokelewa na Mbunge wa Ukerewe Mhe. Mkundi na kupokelewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Madiwani, katika MSAFARA huo Mhe. Mbowe ameongozana na Mbunge wa Bunda, Mhe. Ester Bulaya.

Akiwa Ukerewe Mhe. Mbowe amefanya Kikao cha ndani na kuongea na wanachama na viongozi mbalimbali.

Huu ni mwendelezo wa ziara iliyoanza Kanda ya Kati, kisha kuelekea Kanda ya Kusini baadae Kanda ya Nyasa na sasa ni Kanda ya ziwa, ikiwa na lengo la kuangalia Uhai wa Chama mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, kufungua matawi mapya, kuvuna wanachama wapya na kuangalia changamoto mbalimbali zilizopo kwa sasa na kuhakikisha zinafanyiwa kazi.

Akiwa Ukerewe Mhe. Mbowe ameunda Kamati maalum (Task-force) ambayo itakuwa na kazi maalum ya kuhakikisha chama kinakuwa Imara kuliko wakati wote mwingine.

"Niwapongeze sana wananchi wa Mwanza kwa kazi kubwa mnayoendelea kuifanya na kuipigania haki na Demokrasia inayokandamizwa, msikatishwe tamaa, endeleeni kuwa na matamanio ya kushika dola na hilo ndilo tamanio la wengi kwa sasa mabadiliko hayakwepi, hili ni tendo linaloendelea duniani kote, watu wanapohitaji mabadiliko huwezi kuyakwepa, ni muda kidogo umebaki, ni suala la muda tu, hofu zimeshawajaa, hawajiamini, kilichobaki wanatumia nguvu za kijeshi, Mahakama na mamlaka mengine kukandamiza Upinzani, linatokea kwa Mbunge wa Arusha mjini, Mhe. Godbless Lema na tumeahuhudia juzi Mbunge wa Kilombero Mhe. Lijualikali akihukumiwa miezi 6 kwenda jela, hii ni Vita kati ya ccm na Upinzani hakuna kingine, shime na sisi tuko ngangari harudi mtu nyuma, lazima tuipiganie haki, nchi iendeshwe kwa kufuata Katiba na Sheria zake, Rais aliapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania" amesema Mhe. Mbowe.
 
Tumaini is good hata wakristo mpaka leo wanatumain yesu atarudi tena miaka 2017. Na Chadema huenda wakasubiri hayo matumaini muda mrefu. Ila haki haiombwi huwa inachukuliwa kwa gharama yeyote ile. Kama wanahaki chukueoni
 
Back
Top Bottom