Queen V
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 775
- 1,332
Kiongozi wa Upinzani Bungeni Freeman Mbowe wakati akiijadili hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ameliambia Bunge kuwa msimamo wa Kambi ya Upinzani ni kumtaja hadharani na kumshutumu mtu yeyote ambaye alishiriki ama anashiriki katika kulihujumu Taifa bila kujali kama yupo Serikalini ama Kambi ya Upinzani.
Kiongozi huyo mkuu wa kambi hiyo ya upinzani amesema hayo kufuatia wabunge kupitia chama cha mapinduzi kumshutumu aliyekuwa Waziri mkuu wakati uuzaji wa nyumba hizo za Serikali Frederick Sumaye ambaye sasa ni mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA kuwa naye alishiriki katika uuzaji wa nyumba hizo kwani Rais wa sasa Dr.John Magufuli alikuwa waziri wa ujenzi na Sumaye alikuwa bosi wa Dr. Magufuli kama Waziri Mkuu.