Mbowe anyemelewa na TRA mkoa wa Kilimanjaro, Apewa siku 14 kulipa kodi Tsh 13.5m

Mugabe one

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
2,327
1,684
Freeman Mbowe akiwa ni mmiliki wa Protea hotel anadaiwa hajalipia service levy kwa miaka 5, huko wilayani HAI, kapewa Siku 14 alipe deni hilo na fidia.

Pia TRA Kilimanjaro hajawahi kupeleka audit report kwa miaka 10 kinyume cha sheria, hivyo amekuwa akikwepa kodi TRA.

-------------
Mbowe.png


Miezi takribani mitano iliyopita tangu aondolewe Billcanas, siku moja tangu Serikali imzuie asiendelee na shughuli za kilimo katika shamba lake, Mwenyekiti huyo wa Chadema amepewa siku 14 awe amelipa kodi inayokadiriwa kufika milioni 13.5, ya hoteli yake ya Aishi iliyoko Machame Mkoani Kilimanjaro.

Uamuzi huo mpya wa Serikali wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro,umefikia hatua hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Gellasius Byakanwa, kutangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Veggies analomiliki Mbowe kutokana na kile kilichosema lipo ndani ya chanzo cha maji.

Byakanwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano imelenga kukusanya mapato ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwamo kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Hatuwezi kufikia malengo ya ukusanyaji mapato yetu ya ndani kama kuna wafanyabiashara wakubwa kama huyo wanakwepa kulipa kodi, na tena kwa kipindi chote hicho ameshindwa kuleta hali ya mauzo yake ambayo yataweza kujulikana kiasi anachostahili kulipa kodi,”amesema Byakanwa.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amemshutumu Mbowe kwa kufanya uharibifu wa mazingira kwa kuvuna miti ya asili bila kibali cha mkuu wa Wilaya kulingana na uamuzi wa Kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na kuvuta maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za utumiaji wa maji mfereji.

Chanzo: Dar24
 
Freeman Mbowe akiwa ni mmiliki wa Protea hotel anadaiwa hajalipia service levy kwa miaka 5, huko wilayani HAI, kapewa Siku 14 alipe deni hilo na fidia,
Pia TRA KILIMANJARO hajawahi kupeleka audit report kwa miaka 10 kinyume cha sheria, hivyo amekuwa akikwepa kodi TRA.
SHIKAMOO KAKA MBOWE.


Mbowe, Lowasa, Lisu, Zito Kabwe ndiyo adui Namba 1 wa Watanzania!
 
hizo media siku hizi ni za propaganda ya serikali hazina ushawishi.kwa wenye mawazo huru.
Muulize DED HAI, AU MANAGER WA TRA KILIMANJARO KAMA HUWEZI UKAVIAMINI VYOMBO HOVYO AU USUBIRI GAZETI LA MTANZANIA DAIMA LA MBOWE ILI ULIAMINI VIZURI AKUAMBIE USITUMIE KUPIGIA KURA KALAMU ZA NEC ALAMA ITAHAMIA KWA MGOMBEA WA CCM, VERY GOOD
 
Muulize DED HAI, AU MANAGER WA TRA KILIMANJARO KAMA HUWEZI UKAVIAMINI VYOMBO HOVYO AU USUBIRI GAZETI LA MTANZANIA DAIMA LA MBOWE ILI ULIAMINI VIZURI AKUAMBIE USITUMIE KUPIGIA KURA KALAMU ZA NEC ALAMA ITAHAMIA KWA MGOMBEA WA CCM, VERY GOOD
mkuu vitu kama hivyo document zinaongea sio uliowataja.Tanzania Daima sijawahi nunua.nasoma Mwananchi/balanced media house.
 
Back
Top Bottom