Chabruma
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 5,660
- 1,777
CHADEMA sasa wameufyata kwa Lowassa. Kawazunguka kila kona mpaka wanashindwa kupumua. Lile jinamizi ambalo liliikumba CCM sasa limehamia CHADEMA. CHADEMA sasa hawana uwezo wala nguvu ya kumwajibisha Lowassa.
Lowassa anaendelea na mikakati ya kujiimarisha ndani ya chama hicho ili ifikapo mwaka 2018, aweze kuwa Mwenye Nguvu ndani ya chama. Hili linafanyika kwa kuwarubuni wale wote wenye ushawishi ndani ya chama. Alianza kumchukua Salum Mwalimu kuwa ndiye mpiga debe wake. Sasa kahamia kwa Katibu Mkuu Vincent Mashinji kwani anaamini kuwa ndiye mtendaji wa chama hata kama uwezo wake wa kuongoza ni mdogo.
Freeman Mbowe ameiona hali hiyo na haridhishwi nayo. Naye anafanya mikakati ya kung'ang'ania kiti. Hataki kumuachia Lowassa hata kama amepewa pesa nyingi. Anataka aendelee kuwa Mwenyekiti ili kulinda heshima yake na ya wenye chama.
Suluhu inatafutwa chumbani. Naam si nyingine ni ile ya kucopy na kupesti katiba ya msaliti wao, Zitto Kabwe wa ACT. Kwamba ili Lowassa andelee kuwa mfalme ndani ya CHADEMA kwa vile hawana uwezo wa kumzuia asigombee Uchaguzi Mkuu wa 2020, atafutiwe cheo kingine ambacho kitaonekana ni kikubwa ndani ya CHADEMA kuliko cha Mwenyekiti. Hivyo Lowassa atakuwa Kiongozi Mkuu wa CHADEMA na Mbowe atabaki kuwa na cheo chake cha Mwenyekiti. Hiyo ndiyo suluhu inayotafutwa na ni maelekezo ya Lowassa.
Tutaona mengi