Mbowe amlipua JK

Mfano ni wewe mwenyewe umekana kauli zako nyingi na unajikanganya sana
 

Sauti ya umma Ni sauti ya Mungu....Mh Mbowe anasimamia kauli ya Umma ambayo Mh Warioba aliiwakilisha kupitia Rasimu ya Katiba. Hivyo wanaoipinga kauli hii ya umma, Ni wale Tu wanaoongozwa na mkono WA shetwani...na ndio mhimili WA uovu ambao CCM imejishikiza. Kuupinga umma Ni kumpinga Mungu, na mpinzani WA Mungu kwa vizazi na vizazi Ni ibilisi, na CCM inasimama ktk mstari huo muovu ILA itashindwa na kutupwa ktk abyss, yaani shimoni kama shetwani, na ndiko tuendako sasa na CCM hii! Watanzania walishaamua, walishafikia mwisho WA maamuzi Yao. Katiba mpya inayowafaa ndio jibu sahihi. Anayeipotosha, kuipinga au kuihujumu hastahili kuwepo ktk historia ya Tanganyika mpya!
 
hakafu mbona presidaa alisema hadi jumanne majina ya wabunge la katiba atakuwa kashayataja?sasa ishapita siku moja tayari
 
Mbowe angeenda shule asingeongea huu ujinga hapo juu! Shule inasaidia sana, hata uwe na fedha vipi kama hujaenda shule huwezi kuwa na hoja iliyosimama ipasavyo!

kwahiyo elimu yako wewe ndio ya kujiita msalani nyie mliozaliwa kupitia masabuli mna tabu.
 
Lakini kweli kuna mara nyingi waandishi wetu uwanukuu vibaya (au kwa makusudi)...
Yes, lakini tukubaliane mara nyingi sana wanasiasa wetu wengi ni wabovu sana katika kufikiria athari au matokeo ya kile wanachokisema katika jamii na hii inatokana na ukosefu wa taaluma au experiance katika mawasiliano na sheria.

Ukiangalia nchi zilizoendelea ambazo tunataka tuwe kimaendeleo kama wao, utagundua kuwa wanasiasa wengi wazuri kihoja, kimantiki na vision ni wataalam wa sheria, sayansi ya siasa na kiuchumi.

It makes a lot of sense and big difference to our politics.
 
Mfano ni wewe mwenyewe umekana kauli zako nyingi na unajikanganya sana
Watendee haki kihoja wasomaji wa bandiko lako hii hapa Jf kwa kuziainisha kauli zangu ambazo nimejikanganya.
 
Wanaopinga wana haki iliyosawa na wale wasiopinga kwa sababu maoni yao kama binadamu hayatofautiani katika macho ya mwenyezi Mungu. Kwani si tunaambiwa kuwa Mungu anawapenda wanae wote na wote kwake wako sawa! Itakuwaje tena wana wa Mungu wawe wanaongozwa na mkono wa shetani wakati Baba yao yupo kila sekunde katika njia zao!.
 

JK nilikuwa namkubali sana alivyoanza kwenye mchakato wa kutafuta katiba mpya, lakini inaonekana makada wa CCM wamemkalia kooni sn na kuanza kuropoka kama akina Kinana na wenzake.,

Ni vyema angebaki kimya na zaidi akawataka na kuhimiza watu kwenye bunge la katiba wachangie vyema ili kupata katiba itakayowafaa watanzania wote wakiwemo na wasio na vyama., lakini kuja kwenye majukwaa na kutamka chama changu kinataka serikali 2 hapa amefanya ujuha wa hali juu kabisa.,

Sasa kama chama chako kinataka mfumo wa serikali 2 kwanini uliruhusu mchakato wa katiba mpya na serikali 2 zipo sasa?? ilikuwa tuendelee nazo tu, hawa CCM ovyo sana wanaogopa na kutishana tishana hata Rais anakuwa hana mamlaka lazima afuate na kuburuzwa na watu wachache hii nchi bado sn.,
 
Tatizo la Mbowe ni shule.

huhitaji shule kujua tume ya katiba ilichokuwa inakifanya kunahitajika uwazi zaidi kwa kuwa suala linagusa wananchi ambao ndio wameamua serikali tatu , kusimamia hotuba za mwalimu kwa karne hii ni kufilisika kisiasa zilikuwa na mashiko wakati huo sio sasa la msingi si hoja ni kusimamia utashi wa wananchi katiba sio ya ccm ni kwa ajili ya nchi na taifa kwa ujumla wenye ,mamlaka ya kukataa viongozi ni wananchi sauti zao zisipuuzwe idumu tanzania
 


Ni kweli unachosema,ila nilitaka uhakika kama mbowe asema neno'NGUMI' .
 
Mwambieni MBOWE aache kulalamika majukwaani, wafunde Wabunge wake waende DODOMA wakiwa na hoja badala ya ujinga ujinga tena.

kama Lisu akitolewa nje ya bunge kisa ANACHANGIA SANA je?nao ni ujinga ujinga?
 
Sina hakika kama umefikiri vizuri ulipoandika maneno niliyowekea rangi .Hotuba za Nyerere zilikuwa zinafichua mambo ya mbele zaidi hata kabla ya karne kufikiwa. Hili halionekani na mimi peke yangu linaonekana hata na wazuoni wengine. Mifano ya aliyoyasema yakaonekana baadaye ni mingi, lakini kwa kukusaidia nitaje michache. Ukiona mtu anakimbilia Ikulu, mwogope kama ukoma. Waliokimbilia Ikulu hatukuwagopa matokeo tumeyaona.
Dhambi ya ubaguzi ukiianza haitakuacha. Mtaendelea kubaguana. Tumeiona Sudani kusini.
Lakini nisikulaumu sana kwa sababu kufikiri vizuri sio jambo jepesi ingawaje kila mtu huwa anafikiri. Lakini hata kama utafikiri vizuri kukumbuka pia ni jambo gumu huwenda unashindwa kuyakumbuka aliyoyasema Nyerere yaliyombele ya wakati hadi sasa. Hata wanaodai serikali tatu ni wale waliokwisha sahau mawazo yake kuwa huo nia aina ya ubaguzi unaotokana na ulevi tu hasa ulevi wa madaraka. Kutaka bendera, wimbo wa taifa kupigiwa mizinga. Nyerere alisema Rais achaguliwe kwa sifa alizonazo na sio kabila lake. Anazo sifa zooote, lakini Ahh! Mkara. Hana sifa hata moja ya kuwa Rais lakini mimi namtaka Seif Sharif Hamad. Kwa nini? Mpemba bwana.
Haya ndiyo yanayofanyika sasa miaka 14 baada ya kifo chake. Nani kapitwa na wakati? Nani kafirisika kisiasa?
 
Wenzetu pia wanasaidiwa na uwazi uliopo. Ukidai umenukuliwa vibaya, chombo hicho cha habari inatia mkanda na kulinganisha kauli yako na madai yako. Huku kwetu mwanasiasa akisema amenukuliwa vibaya anasaidiwa kuficha ukweli na kukazia ukanushaji wake huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…