Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Ni kweli ilitakiwa awe na kibali........hamna kudhalilishana wala nini kibali muhimu.
Hivi kinyume na taratibu ni uvunjaji wa sheria.. nilitegemea wangesema amevunja sheria no. flani sio kuja na hija zisizo za msingi.Polisi wamkamata Mbowe, ahaojiwa na kuachiwa
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi, ni kwamba mbunge huyo alifanya hivyo kinyume na taratibu na pasipokuwa na kibali kutoka kwa jeshi hilo.
Nipashe
Taratibu zinasema kwamba ukitaka kupiga fataki ni lazima kutoa taarifa polisi ili upewe kibali.Ni Tanzania tu ambapo watu wanajifanyia mambo ovyo ovyo. Si haki kwa mtu kukupigia fataki saa nne usiku bila taarifa
Lol! Serikali hii kwa visa utadhani mama mkwe! Wale wahindi walikuwa na sikukuu sijui ya nani huko wakapiga fataki hadi watu wakadhani imekua zamu ya mabomu ya kigamboni kulipuka; walichukuliwa hatua gani? Double stds at work,lol
Uvivu mbaya sana!!Kumbe mambo mengine yakujitakia ngoja anyee debe ajifunze siku ingine kufanya mambo kwa utaratibu
Taratibu zinasema kwamba ukitaka kupiga fataki ni lazima kutoa taarifa polisi ili upewe kibali.
Hazisemi ukawaambie majirani.
Stuka.
Ninamashaka na upeo wako wa kufikiri. Hizi chuki binafsi zitawaua kabla ya wakati wenu....Kumbe mambo mengine yakujitakia ngoja anyee debe ajifunze siku ingine kufanya mambo kwa utaratibu
Hivi kinyume na taratibu ni uvunjaji wa sheria.. nilitegemea wangesema amevunja sheria no. flani sio kuja na hija zisizo za msingi.
Ukweli nikwamba jeshi la polisi limejisahau, kama kupiga fataki ni kosa mbona zinauzwa madukani kiholela na kila mwenye uwezo anajinunulia na kuzipiga atakavyo?? Siku mambo yatabadilika nchi hii ndio watajua jukumu lao kwa raia.
Taarifa polisi inasaidia nini kama watakaosumbuliwa hawatapewa taarifa ya usumbufu tarajiwa?Kimsingi ni kuwa, anaekupa kibali ndie anaetakiwa kutoa taarifa kwa majirani kuwa kutakuwa na jambo kadha wa kadha