Mbowe achia chama kwa vijana wakijenge la sivyo 2020 yatawakuta makubwa CHADEMA

KATASAN'KAZA

JF-Expert Member
Jul 24, 2013
3,097
1,352
Nianze kabisa na kauli ya mzee Sumaye wakati anatimuka CCM alisema haichukii CCM ila amekwenda upinzani kuongeza nguvu ili nchi iwe na siasa zenye uzani linganifu kwa kiasi fulani.

Binafsi licha ya kuwa kulikuwa na advantage ya kisiasa hasa ukilinganisha na wakati anahama CCM ila binafsi nilimwelewa kwa kauli yake badala ya kuangalia mchango wake kwa uchaguzi uliokuwa habari ya Tanzania muda ule.

Point yangu kwa mh. Mbowe ni moja tu, siasa ni kama mchezo wa mpira timu humwajiri kocha ili kushinda kikombe na kocha huyo hupewa muda kwa maana ya mkataba akishindwa kutimiza malengo kama ni muungwana hutundika madaruba au kama si muungwana basi kutimuliwa huwa zawadi pekee ambayo huzawadiwa na waajiri wake.

Kwa siasa za CHADEMA kama ilivyo kwa mchezo wa soka ni wazi uwezo wa Mbowe kuipatia nguvu zaidi umeisha na kitakachofuatia ni kuiporomosha bila shaka na mbaya zaidi itakuwa ni kabla ya 2020.

Ushauri wa bure kwa viongozi wa CHADEMA hasa mwenyekiti wake mh.Mbowe ni muda mwafaka kuruhusu vijana kuongoza chama simaanishi wazee hawatakiwi ila kwa mwendo wa siasa za sasa hapa nchini ni wazi vijana watafanya vizuri kuliko wazee kwa tafiti za kijamii maana vijana ni wengi katika mwitikio wa kisiasa na ni wazi ushawishi wa vijana kwa vijana wenzao ni mkubwa kuliko ushawisho wa wazee.

Niliwahi kuwasihi viongozi wa CHADEMA juu matumizi ya mtaji wa vijana hasa katika kujenga chama ila badala yake naona viongozi wanaona fahari kuwafanya mtaji wa kuongeza umaarufu wa chama.

Narudia tena CHADEMA na hasa mh. Mbowe ukiendelea kudharau mchango na mtaji wa vijana katika kujenga upinzani haitakuwa shida kuona upinzani unakufa hasa kwa chama km chadema hasa baada ya kuona vijana hawathaminiwi katika kutoa mchango wao katika siasa za chama.

Nasema wazi kijana wa CHADEMA mwenye nyazifa kichana si kwasababu wanauwezo bali wengi wao ni kuwa wanamaslahi ya kisiasa na viongozi wa chama wa ngazi za juu na pia hapingikii kuwa sura ya undugu na ukabila vinatamalaki na hii ni sura yenye mzizi na ccm. Hali hii haitakiwi kuonekana chedema .

Asanteni wenu kada kindakindaki.
 
Bila shaka ujasoma thread yote km umesoma basi akili zako zinakutosha wewe tuu..
 
Huu wimbo wa ukabila na ukaskazini ulitungwa vyema sana na Maccm na baadhi ya wanachadema wanauelewa sana ila ni wimbo wa kipuuzi tuu

Binafsi Mheshimiwa Mbowe bado ana nguvu kubwa sana ya kukiongoza chama sio sasa tu hata miaka mingi ijayo bado nina imani naye lakini sio kwamba hakuna wanaoweza!
 
Hao vijana waende wakaunde chama chao kama ni rahisi hivyo au onyesha ni chama gani TZ, kimeachia chama kwa vijana.
 
Sio swala la kumwachia kijana swala ni kumwachia mtu mwenye uwezo naye akiongoze kwa fikra mpya.
Chadema ina watu wachache katika safu yake wanaoweza acha tuu kuongoza hâta kujenga hoja.
Tafakari niwangapi wanaweza kukaa round table na viongozi wa dunia kujadili mambo makubwa ya kimaendeleo na kiusalama mf.
Bungeni tuu ili wachangie bila kutetemeka wanapiga pombe kwanza sasa kimataifa sindio watakunywa sumu kwanza kukomeshea!
Kimsingi kiongozi ajaye ashughulike na ombwe la wasomi na watu makini katika safu ya uongozi / ubunge chamani.
 
Ndio maana mnaitwa nyumbu,you can't think for yourself at all.Sishangai kuona nyie wote leo mnamkubali Zitto simply because Mbowe anamkubali.Akili za nyumbu hizi.
Naona ushabugia viroba bila msosi
 
Kwa kauli yako mwenyewe umesema CHADEMA ina watu wachache wanaofaa kuongoza.Sasa nani hapo wa kulaumiwa?yaonekana uongozi uliopo umeshindwa kabisa kume_mentor au kuwaandaa watu wa kupokea vijiti,taasisi zote imara huwa na utaratibu mzuri wa kuandaa viongozi wake,tangu wakiwa na umri mdogo.Hainiingii akilini leo mkisema eti haiwezekani kuwapa wengine nafasi za kuongoza kwavile hawaaminiki,come on! Kama kweli kuna tatizo hilo ndani ya CHADEMA basi wa kulaumiwa ni hao viongozi wenu maana yaonekana dhahiri mipango yao ya kuijenga chama haihusishi political future ya CHADEMA.Au labda wanafanya hivyo kwa makusudi ili wapate kisingizio cha kuendelea kuitawala CHADEMA,Mimi binafsi siamini kama hakuna makada wenye uwezo wa kumrithi Mbowe, wapo wengi tu na tena wana uwezo mkubwa kuliko Mbowe ila wanaogopa kuchafuliwa mara wakatapotangaza kuwania nafasi ya Mwenyekiti,wengi wao wana heshima kubwa ktk jamii kutokana rekodi zao nzuri za utumishi ktk sekta ya umma,sekta binafsi na mashirika/taasisi za kimataifa.Wasingependa waharibiwe heshima zao walizozijenga kwa miaka mingi sana,na kwasababu hii CHADEMA wataendelea kupoteza fursa ya kukosa michango ya kiutumishi kutoka kwa watu wenye uwezo wa kweli wa kukifikisha chama mbali zaidi kisiasa.
Sio swala la kumwachia kijana swala ni kumwachia mtu mwenye uwezo naye akiongoze kwa fikra mpya.
Chadema ina watu wachache katika safu yake wanaoweza acha tuu kuongoza hâta kujenga hoja.
Tafakari niwangapi wanaweza kukaa round table na viongozi wa dunia kujadili mambo makubwa ya kimaendeleo na kiusalama mf.
Bungeni tuu ili wachangie bila kutetemeka wanapiga pombe kwanza sasa kimataifa sindio watakunywa sumu kwanza kukomeshea!
Kimsingi kiongozi ajaye ashughulike na ombwe la wasomi na watu makini katika safu ya uongozi / ubunge chamani.
 
Sio swala la kumwachia kijana swala ni kumwachia mtu mwenye uwezo naye akiongoze kwa fikra mpya.
Chadema ina watu wachache katika safu yake wanaoweza acha tuu kuongoza hâta kujenga hoja.
Tafakari niwangapi wanaweza kukaa round table na viongozi wa dunia kujadili mambo makubwa ya kimaendeleo na kiusalama mf.
Bungeni tuu ili wachangie bila kutetemeka wanapiga pombe kwanza sasa kimataifa sindio watakunywa sumu kwanza kukomeshea!
Kimsingi kiongozi ajaye ashughulike na ombwe la wasomi na watu makini katika safu ya uongozi / ubunge chamani.
Mchango mzuri huu
 
Nianze kabisa na kauli ya mzee Sumaye wakati anatimuka CCM alisema haichukii ccm ila amekwenda upinzani kuongeza nguvu ili nchi iwe na siasa zenye uzani linganifu kwa kiasi fulani.

Binafsi licha ya kuwa kulikuwa na advantage ya kisiasa hasa ukilinganisha na wakati anahama ccm ila binfsi nilimwelewa kwa kauli yake badala ya kuangalia mchango wake kwa uchaguzi uliokuwa habari ya Tanzania muda ule.

Point yangu kwa mh. Mbowe ni moja tu, siasa ni kama mchezo wa mpira timu humwajili kocha ilikushinda kikombe na kocha huyo hupewa muda kwa maana ya mkataba akishindwa kutimiza malengo km ni muungwana hutundika madaruba au km si muungwana basi kutimuliwa huwa zawadi pekee ambayo huzawadiwa na waajili wake.

Kwasiasa za chadema km ilivyo kwa mchezo wa soka ni wazi uwezo wa mbowe kuipatia nguvu zaidi umeisha na kitakachofuatia ni kuiporomosha bila shaka na mbaya zaidi itakuwa ni kabla ya 2020.

Ushauri wa bure kwa viongozi wa chadema hasa mwenyekiti wake mh.Mbowe ni muda mwafaka kuruhusu vijana kuongoza chama si manishi wazee hawatakiwi ila kwa mwendo wa siasa za sasa hapa nchini ni wazi vijana watafanya vizuri kuliko wazee kwa tafiti za kijamii maana vijana ni wengi katika mwitikio wa kisiasa na ni wazi ushawishi wa vijana kwa vijana wenzao ni mkubwa kuliko ushawisho wa wazee.

Niliwahi kuwasihi viongozi wa chadema juu matumizi ya mtaji wa vijana hasa katika kujenga chama ila badala yake naona viongozi wanaona fahari kuwafanya mtaji wa kuongeza umaarufu wa chama.

Narudia tena CHADEMA na hasa mh. Mbowe ukiendelea kudharau mchango na mtaji wa vijana katika kujenga upinzani haitakuwa shida kuona upinzani unakufa hasa kwa chama km chadema hasa baada ya kuona vijana hawathaminiwi katika kutoa mchango wao katika siasa za chama.

Nasema wazi kijana wa chadema mwenye nyazifa kichana si kwasababu wanauwezo bali wengi wao ni kuwa wanamaslahi ya kisiasa na viongozi wa chama wa ngazi za juu na pia hapingikii kuwa sura ya undugu na ukabila vinatamalaki na hii ni sura yenye mzizi na ccm. Hali hii haitakiwi kuonekana chedema .

Asanteni wenu kada kindakindaki.
Huu ushauri wapelekee CCM waache kunang'ania madaraka zanzibar mbowe bado kijana na ana nguvu kubwa tu kwani umemuona bungeni kalala kama nape?
 
Back
Top Bottom