ALWATAN KIZIGO
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 539
- 642
Na
Augustine Chiwinga.
Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa CHADEMA , chama kinachoamini katika itikadi ya UBEPARI.
Kwa elimu kidogo juu ya itikadi ya UBEPARI ni mfumo unaomini katika unyonyaji baina ya mtu na mtu na ni mfumo unaoamini katika matabaka kati ya WAVUJA JASHO NA WAVUNA JASHO.
Na kutokana na itikadi hiyo ya CHADEMA ndio maana mwenyekiti wao taifa hakuona hatari kuanzisha shamba lenye takribani hekari 30 katika chanzo tengefu cha maji ya mto Weru Weru ambao unategemewa na wakazi 210,533 wa wilaya ya Hai.
Chanzo cha maji cha mto Weru Weru ni eneo tengefu mtu yeyote haruhusiwi kuendesha shughuli za kiimo au ujenzi pale lakini Mbowe kwa jeuri akavunja sheria hii ya serikali na kwenda kuanzisha shamba ambalo kwa siku lilikua linatumia lita nyingi za maji kumwagilia mazao yake jambo lilliloababisha chemchem kukauka na maji kupungua sana.
Pamoja na hayo Mbowe alikua anatumia madawa ya kemikali yakuua wadudu kwenye shamba lake ambapo dawa zile zilikua zinaenda moja kwa moja kwenye maji ya mto huo hivo kuhatarisha maisha ya malaki ya watu wanaotumia maji hao.
Kutokana na uharibifu aliokua anaufanya Mbowe kiwango cha kemikali ya Nitrate imeongezeka kwenye maji hayo na kufikia Miligramu 26 kwa lita kemikali hii ni hatari kwa sababu hudhoofisha uzalishaji wa insulin na kusababisha ugonjwa wa kisukari na magonjwa mengineyo ya hatari.
Lakini pia takwimu za kitaifa za rasilimali za maji zilizopo zinaonesha kwamba kiwango cha upatikanaji wa maji kwa kila mtanzania ni mita za ujazo 1,952 kwa mwaka na endapo juhudi za kulinda vyanzo vya maji zisipochukuliwa,kiwango hicho kinatarajiwa kushuka hadi kufikia mita za ujazo 883 mwaka 2035 na ndio maana wizara ilitenga eneo la mto Weru Weru kua eneo nyeti ili kukilinda na kuuia kushuka kwa kiwango cha upatikanaji wa maji kwa nchini.
Lakini inashangaza kiongozi mkubwa aliyekabidhiwa dhamana ya kua mwenyekiti wa Chadema taifa na kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni kaka yangu Freeman Mbowe anafanya mambo ya aibu na hatari namna hii kwa wananchi anaowaongoza wa wilaya ya Hai hakika huyu sio kiongozi bora .
Kukausha chanzo cha maji kwake si kitu cha maana kilicho bora kwake ni mradi wake wa shamba ambao unanufaisha familia yake binafsi na sio malaki ya watu wanaotegemea maji hayo.
Namshauri Mbowe na wapambe wake waache kueneza maneno ya kwamba wanaonewa , ilihali wao ndio wanawaonea wananchi wa Hai kwa kuwadhulumu maji yao ya Weru Weru hivo aondoke na kuachia eneo hilo kwa sababu eneo hilo linalindwa kisheria na yeye hana uhalali wa kuendelea kuendesha shughuli za kiimo maeneo yale.
Nampongeza DC wa wilaya ya Hai Mh Gelasius Gaspa Byakanwa kwa moyo wake wa kizalendo na kujitolea kulinda na kutetea maslahi ,ustawi na uhai wa wana Hai .MUNGU ambariki sana hakika Mh Rais hakukosea kukuchagua katika nafasi hiyo.
Augustine Chiwinga