Mbongwe Nsoga yawafariji wagonjwa MOI

Mbongwe Nsoga yawafariji wagonjwa MOI

Joined
Apr 15, 2025
Posts
91
Reaction score
174
Kampuni ya ushonaji nguo ya Mbogwe Nsoga imewafariji wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kwa kuwapatia zawadi ya nguo.

Faraja hiyo imetolewa leo Januari 11, 2026, wakati kampuni hiyo ilipotembelea MOI ikiongozana na Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Jimbo la Mbogwe, Mkoa wa Geita, Mhe. Ferguson Nkingwa, kwa lengo la kuwafariji na kuwatia moyo wagonjwa.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mhe. Nkingwa amesema kuwa asilimia kubwa ya wagonjwa waliopo MOI ni majeruhi wa ajali, ambapo wengi wao wanatoka katika familia zenye kipato cha chini, hali inayowafanya washindwe kumudu mahitaji ya msingi wakiwa wodini.

“Tumekuja hapa MOI kwa kushirikiana na kampuni ya Mbogwe Nsoga ili kuwafariji wagonjwa. Tumewapatia nguo mbili hadi tatu kwa kila mgonjwa kuanzia wodi za watoto, watu wazima, ICU pamoja na HDU,” amesema Mhe. Nkingwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbogwe Nsoga, Bw. Peter Deus, amesema kuwa kampuni hiyo inatambua mahitaji makubwa ya wagonjwa waliolazwa hospitalini, jambo lililoisukuma kutimiza ahadi yake ya kufanya tendo la huruma.

“Kama kampuni, tuliahidi siku moja tutafanya jambo la kuwafariji wagonjwa, na leo tumeanza kutekeleza ahadi hiyo hapa MOI,” amesema Bw. Deus.

Naye mmoja wa wanufaika wa faraja hiyo, Bi. Asha Juma, ameishukuru kampuni hiyo kwa kujitolea na kuonesha upendo kwa wagonjwa waliolazwa wodini.

“Tunawashukuru sana kwa kutuona na kutufariji. Tunaomba muendelee na moyo huo wa kusaidia hata wengine wenye uhitaji,” amesema Bi. Asha.
img-20260111-wa0067-jpg.3528690
 

Attachments

  • IMG-20260111-WA0067.jpg
    IMG-20260111-WA0067.jpg
    784.2 KB · Views: 18
  • IMG-20260111-WA0066.jpg
    IMG-20260111-WA0066.jpg
    728.1 KB · Views: 10

Similar Discussions

Back
Top Bottom