Mbona wabunge wa upinzani tu ndi wanakomaliwa na spika?

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
17,342
21,443
Ukifuatilia vikao vya bunge vinavyoendelea mjini dodoma utakuta kama wabunge wa upinzani pekee ndio wanaonekana kukomaliwa na kiti cha spika,mara utasikia ameambiwa afute kauli,au amepewa siku kadhaa andike barua ya kujieleza,je makosa haya wabunge wa chama tawala wapo sahihi kwa kila walisemalo
 
Sasa wapi wabunge wa chama tawala wanabebwa tu hata wakiongea mbovu spika na nanaibu wake wanajikausha kama hawajasikia .Yaani hiyo ni mikakati tu kuwarudisha nyuma wapinzani au kukatisha tamaa upinzani hakuna kukata tamaa mwendo mdundo .Mungu yupo kila kitu kina mwanzo na mwisho hata uhai wa binadamu unamwisho wake ipo siku watu hawataamini ni kuomba uzima siku hazigandi.
 
Katiba! Katiba! Katiba! Katiba! Tulilie Katiba Mpya.Pawepo na ibara isemayo; "Spika wa Bunge asitokane na chama chochote chenye uwakilishi bungeni." Bila ya hivyo tutaendelea na hii 'status quo' mpaka hapo tutakaporudi kwenye 'drawing board'.
 
Hio umeiona pengine wapi duniani. Chama unachokitetea kikiongoza wabunge unafurahia. Majuzi kati tu mapovu yamewatoka wapinzani kuhusu umeya dar mbona hukushauri awepo Maya asie na chama?
 
Hivi mkuu,mbona mmemezwa sana na haya mavyama ya siasa? Nani kakwambia ukishauri au kukosoa lazima uwe na itikadi ya chama? Si kila mtu humu ana huu upuuzi wa kusujudia itikadi za vyama.Tuangalie hoja na si kuhusisha kila suala na chama.
 
kweli, wengi wao waliokotwa tu mtaani, hawajawai fanya kazi yoyote ya kitaalamu, hawajui taratibu, zaidi ya yote ni wasanii, niliruhu niwataje kwa majina moja noja
 
Kwanini yule aliyesema ili upate ubunge viti maalum upinzani lazima uwe beibi wa wakubwa Chamani asingeambiwa athibitishe kauli hiyo?
 
Hapa kubwa ni katiba lakini kiti cha spika kama kajiushabiki kwa mbali
 
Kwanini yule aliyesema ili upate ubunge viti maalum upinzani lazima uwe beibi wa wakubwa Chamani asingeambiwa athibitishe kauli hiyo?
Athibitishe nn wakati kubenea aliwahi kusema kua wabunge wao wamevuliwa chupi na shanga. Sasa jiulize kubenea alijuaje kama wamevuliwa wakati pale ukumbini hakukua na chupi wala shanga
 
Katiba! Katiba! Katiba! Katiba! Tulilie Katiba Mpya.Pawepo na ibara isemayo; "Spika wa Bunge asitokane na chama chochote chenye uwakilishi bungeni." Bila ya hivyo tutaendelea na hii 'status quo' mpaka hapo tutakaporudi kwenye 'drawing board'.
Sioni kama utawala wa Bunge hili utakuwa tayari kuanzisha tena hilo jambo sidhani.
 
Ukifuatilia vikao vya bunge vinavyoendelea mjini dodoma utakuta kama wabunge wa upinzani pekee ndio wanaonekana kukomaliwa na kiti cha spika,mara utasikia ameambiwa afute kauli,au amepewa siku kadhaa andike barua ya kujieleza,je makosa haya wabunge wa chama tawala wapo sahihi kwa kila walisemalo
Hawa wabunge wa chadema na chama chao ni kikundi cha makambale hawana adabu ndani ya chama hata nje ya chama.
Na wewe unayeshangaa sijui nawe unafikiria kama wao. Wakijirekebisha hawatapata misukosuko. Kubenea ni mzee wa uongo
 
Hivi kuna watu waongo kama CCM,Nape kadanganya kuhusu kurusha Bunge live hadi sasa hivi hana uongo wa kudanganya tena,Makonda kadanganya kua watu wameficha sukari lakini hadi sasa amna aliefikishwa mahakamani kwa kosa la kuficha sukari.Sasa niambie ni nani muongo
 
Katiba mpya ndio mpango mzima...inatakiwa spika,naibu spika pamoja na mwenyekiti wa bunge wasiwe na itikadi au wasitokane na chama chochote cha siasa! Pia wasiwe na wadhifa mwingine kisiasa wachaguliwe au wateuliwe kwa kuangalia taaluma zao na weledi zaidi!
 
L
Katiba mpya ndio mpango mzima...inatakiwa spika,naibu spika pamoja na mwenyekiti wa bunge wasiwe na itikadi au wasitokane na chama chochote cha siasa! Pia wasiwe na wadhifa mwingine kisiasa wachaguliwe au wateuliwe kwa kuangalia taaluma zao na wOtherwise lazaidi!
Sawa na kusema Rais wa TFF asiwe na ushabiki wa ama simba au yanga. Mtu asiye na itikadi utamjuaje au una kipimo gani cha kujua itikadi? Spika akiwa si mbunge itakuwa afadhali kidogo lakini kumbuka atahitaji kupigiwa kura na wabunge ili awe spika, na kama hivyo ndivyo, kwa vyovyote atajipendekeza kwenye chama chenye majority ya wabunge ili baadaye wamchague tena. Otherwise labda kama utaratibu wa kumpata utabadirishwa badala ya kupigiwa kura.
 
Ukifuatilia vikao vya bunge vinavyoendelea mjini dodoma utakuta kama wabunge wa upinzani pekee ndio wanaonekana kukomaliwa na kiti cha spika,mara utasikia ameambiwa afute kauli,au amepewa siku kadhaa andike barua ya kujieleza,je makosa haya wabunge wa chama tawala wapo sahihi kwa kila walisemalo
baba/mtoto wa mwenye nyumba hakosei!
 
Hio umeiona pengine wapi duniani. Chama unachokitetea kikiongoza wabunge unafurahia. Majuzi kati tu mapovu yamewatoka wapinzani kuhusu umeya dar mbona hukushauri awepo Maya asie na chama?
Kwa hiyo hatuhitaji rasimu ya warioba seriously!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom