Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,334
- 72,798
Kuna nini kimetupata? Nimejaribu kufanya utafiti wangu uchwara na kugundua Watanzania katika kipindi cha nusu nwaka huu furaha haipo kabisa, chuki kati yao iko wazi, hali ya upatikanaji wa huduma kwa wengi imekuwa ngumu, wanasiasa wamekuwa maadui tofauti na zamani wakipokuwa wanabishana kwa hoja, kwenye michezo hakuna kinachoendelea ni aibu tuu nk nk.
Ni kama tuko msibani vile, ndio maana hata sherehe za kitaifa nazo zinazuiwa. Wafanyakazi hata wale waadilifu nao ni woga tuu, huku Polisi nao wameanza kuitwa Gestapo.
Kule kwetu hali hii ya kukosa furaha na mifarakano ikitokea kwenye ukoo tunasema kuna GUNDU. Je, taifa letu nalo limepata GUNDU?