Mambo yaameanza upyaaaa. .......
Visa viroja na vijaruba vya Kasie Mahaba.
Diamond kanisema mie mia ya mia laah naweza sema huu wimbo kanitungia Kasinde mie..... nachojishangaa mbona sikomiii haya mapenzi yana nini? Mbona kuniandama mimi tuu.... au nibatizwe upya!!??
Nilijikuta nimeivuruga password ya ID ya Kasinde kwa sababu ya mahaba haya haya. .....
mwisho wa siku nikatamani sana kuirudia ID yangu..... wapi hadi kesho sijaweza I kumbuka. ....... shkamoo mahaba. Ona sasa mahaba yananipotezea vitu vingi tuu ikiwemo ID yangu kipenzi ya KASINDE ila sikomiii nnini hiki Kasie? ??!!!
Tangu niusikilize huu wimbo najiuliza.... mbona sikomiii licha visa na vijaruba vya mahaba nnavyokutana navyo.
Mara kibao nshajipiga masingi na vibao vya mashavu na kujiambia, Kasie achana na mahaba yanakuumiza, wapi kesho najikuta nna mwingineee. Sisemi kwa sifa bali kiulizo bin mshangao na masikitiko juu.
Mbaya zaidi wao ndo wanaonifata (Kasie be my pilllow and the like..) na hata nikatae vipi wananibembeleza tuu mwisho wa siku aidha nafumania ama nafumaniwa mie.....
Kasie mbona sikomiii. ... sikomiii na siwezi kuachana na mahaba hayaa.
Ngoja nijaribu kuchukua likizo nione kama ntafuzu.
NB: (........................................)
Kama kawaida, wataotoka kapa tafadhali chukua notsi kwa jirani.
Kasie Mahabat Matata.....
Always Smiling.