Mboga imeharibika...

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Posts
20,335
Reaction score
23,951
Ni kwa nini lakini mnatufanyia hivi sisi wakazi wa Kigamboni?

WHY!???

Tangu jana mmekata umeme, mkipigiwa simu ipo busy muda wote mmerudisha leo na kukata kama vile ni taa za christmas tree..mkaamua muukate kabisa...hadi sasa hakuna umeme.

1. Vyakula kwenye friji vimeharibika tayari

2. Ilibaki kidogo tu muunguze na vifaa vya umeme

3. Nguo hazijapasiwa.

WHY US lakini?
Dr F. Ndugulile hili unalifahamu? mbona hakuna uwajibishwaji wowote unaochukuliwa kwa uongozi wa TANESCO Kigamboni?

Hata sitamani kurudi nyumbani na shift yangu hapa kituoni imeisha tangu saa nane...

Mbona hakuna taarifa yoyote kwenye website yao au akaunti yao ya twitter? Walizifungua kwa ajili gani?


Niliuliza kipindi kile cha mvua mwanzoni mwa mwezi Aprili. Kama mvua ile tulikosa umeme siku nne hivi, baada ya kurudi, tulijipangaje kwa mvua nyingine? Jana kamvua ka dakika kumi ndo umeme hadi leo?

This is a big joke..!!!!

Cc: majiyachupa, Mpui Lyazumbi, Kizygote, Paw, Mkulima wa Kuku, mdache, BADILI TABIA, ngalyas_t, Musomakwetu, Manosa ...kama kuna mwenye pasi ya mkaa aniazime tafadhali!
 
Last edited by a moderator:
haha ha haa, hiyo ndo TANESCO inaangaza giza kwa wasio na kisu. #Mentor rudi nyumbani tu usubili hadi operator apate dili la hela na akifurahi atatuwashia. Kwa mwendo huu wa TANESCO tusahau mabadiliko.

Si mmegoma kuondoka kigamboni tutaona hampati umeme hadi muondoke wenyewe... jus kiding
 
hahaha pas ya makaa ! ni muhmu ckuhz,maana taanesco hawaelewek mi cku hz napas za wiki nzma loh
 
hahaha pas ya makaa ! ni muhmu ckuhz,maana taanesco hawaelewek mi cku hz napas za wiki nzma loh

Sasa si ndiyo nilitaka kupasi janaaa...wamekata umeme wanawasha kama taa za krisimasi...on off on off on off aaaaaaargh..very boring people.
 
usiende nyumbani mwae kaa hapohapo, njoo uchukue pesi ila mkaa sina.
 
Kigambon tatizo la kukatwa umeme ni kawaida .
Nilishawahi kuishi huko wanaudhi hao tanesco
 
Kigamboni ilishauzwa mnatafutiwa visa na sababu ili muikimbie
 
wamerudisha sijui saa ngapi!!!
 
Sasa si ndiyo nilitaka kupasi janaaa...wamekata umeme wanawasha kama taa za krisimasi...on off on off on off aaaaaaargh..very boring people.

hehe hii ndo nji yako tanzania uipene kwa moyoowoteee, singin
 
wana kigamboni tumeshazoea migiza na mizenguo ya tanesco,humu hatuhami hata mkisitisha huduma ya kivuko,
 

Unaishi kizungu hafu unataka umeme wa Tanesco, hafu nakushauri tu usipende kununua vyakula vilivyosindikwa itaishia kupata maradhi tu, ingawa wewe unaona ndo maendeleo.
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ! Poleeee! Hama huko njoo huku mchamba wima tunapasia mawe full minyoosho!!
 
Unaishi kizungu hafu unataka umeme wa Tanesco, hafu nakushauri tu usipende kununua vyakula vilivyosindikwa itaishia kupata maradhi tu, ingawa wewe unaona ndo maendeleo.

Sio kusindika mkuu. Jumapili nimepika chakula changu mchana nikajua hiyo mboga hadi jumatatu nikirudi kazini nipike kaugali tu jioni iishe...huoni jinsi ratiba ilivyoharibika!??


Mtaani kwetu tupo na kigogo wa tanesco,
huwa hatujui hata umeme unavyokatika.

Kuuumbe...kuna haja ya kufanya survey ya mahali pa kuishi...

Ha ha ! Poleeee! Hama huko njoo huku mchamba wima tunapasia mawe full minyoosho!!

Nakomaa na jiji Munkari!
 
Last edited by a moderator:
ni mtazamo tuu

hv hawa makampuni ya cm na tanesco hawawez kushirikiana? badala ya haya makampuni ya simu kututumia ma sms ya kijingajinga ucku na mchana ya mabiashara yao ya kutulia pesa zetu,wangetutumia sms zakukatika kwa umeme muda utakapokatwa na kurudishwa. au ndo huo wa kama x mas lights.ili tukae makini na vyombo vyetu na tujipange la kufanya wkt umeme haupo! wapuuz sana hao!and they are not creative.bure kabisa
 
huku kwetu tushazoea jumamosi lazima umeme ukatwe hadi saa moja....

na katikati yawiki lazima umeme ukatwe siku moja mchana kutwa.....

hapo bado zile zima kata zima kata....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…