lowassa is far much better than muungwana na ndio ambayo kidogo alifanya serikali ya JK ....mwaka wa kwanza wafikie mafanikio ambayo yamesimama ghafla especially mafanikio ya shule za kata kila kijiji ...ambayo hadi leo jk anayaimba ..its was lowassa"s baby...hilo halina ubishi...,na ukiondoa kasoro za lowassa ..basi lowassa is better kuliko jk hivi alivyo ....kwani kama utasema labda jk sio fisadi sana ..lakini lazima tujuwe sluggishness yake inaligharimu taifa kiasi gani....
Kuhusu kugombea kwa lowassa sioni kama ni issue kubwa kwani chama kitaamua ..yeye hajatamka tofauti na mtu kama JOHN MAGALE SHIBUDA ambaye yeye kashatamka rasmi interest yake.....
Wakuu zangu jamani mweee!.
Lowassa analindwa na JK kama anavyolindwa Mkapa, Rostam, Karamagi, Meghji, Kingunge na wengineo woote mafisadi wa CCM. Hii ni ilani kuu ya chama pamoja na kwamba haipo ktk maandishi..
Sioni kitu kikubwa kabisa ambacho anatendewa Lowassa ndani ya chama tofauti na wengine hadi hivi sasa kiasi kwamba tufikirie Lowassa anaweza kugombea urais kwa sababu tu anasafishwa ni kutoona mbali zaidi marefu ya mkono..
Hivi kweli watu mnaamini shule za kata ni kazi ya Lowassa toka anaingia Uwaziri mkuu hadi anaondoka kila siku ukifungua gazeti kuna cotoon za Lowassa mara atatuletea mvua za kisayansi, scandal za ndege kupaa, kufukuza kazi waajiriwa,majibu ya kihuni kwa ndugu yetu Mwanakijiji bado tu mnafikira huyu mtu ana nafuu zake kuliko JK ati kwa sababu JK analigharimu Taifa..Sasa ni lipi linatugharimu ambalo halikuwepo wakati Lowassa akiwa PM!
Ama kweli sisi - Miafrika Ndivyo Tulivyo!
Halisi,
Nilisema awali kabisa kuwa kosa pekee tunaloweza kumkamata nalo Lowassa ni Uzembe kutokana na hii Richmond, na zaidi tukitaka sana ni kutumia madaraka na kukiuka kanuni za kazi, jinsi Yona, Mramba na Mgonja walivyofanyiwa.
Lakini tofauti ni kuwa Lowassa, hawawajibishwa kwa uzembe wake wala kulitia Taifa hasara. Alichokifanya kwa kujiuzulu, kimechukuliwa kama adhabu tosha.
Sasa kwa sisi wengine ambao hupima mambo kwa undani, je haya yote ni changa la macho na tangu awali ilikuwa ni makubaliano yao hawa wawili kuwa Kikwete atawale kwa kipindi kimoja kisha amwachie Lowassa au imelazimika kukatisha safari ya Kikwete kwenda kipindi cha pili kutokana na kinachotokea sasa hivi nchini?
Kwenye thread yangu ya mgongano wa Katiba https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kumu-katiba-ya-tanzania-na-katiba-ya-ccm.html nimeuliza ikiwa CCM leo wataridhia kuwa Kikwete hawafai, wanaweza kumvua Uanachama na Uongozi kiurahisi na kuondokana na mfumo wa kiserikali ambao ungeshurtisha Bunge na Mahakama kuu zihusike.
Ni kutokana na udhaifu huu wa kuhakikisha kuna uwajibikaji na Kikwete kukosa Sauti na Mamlaka ndani ya chama, leo hii kina Sitta na Mwakyembe wanatapatapa na kupiga kelele za kuhujumiwa kutokana na haya ya kuonyesha kuwa Lowassa kajipanga vyema na yuko tayari kukichukua Chama mikononi mwake.
Mimi sisikitiki kwa linalotokea CCM, wacha litokee ili tuone sura za kweli za wale wanaodai wao ni Wanamapinduzi na wale wanaotuhumiwa kuwa ni Mafisadi.
CCM kumekuwa na upuuzi na ujinga tangu mchakato wa urais 1995. Na mbaya zaidi ni alichokifanya Mkapa 2005 kwa kufunika Demokrasia kwa ajili ya kutoa upendeleo na kulindana.
Kama Lowassa ataendelea na moto wake wa kutaka Urais ndani ya CCM, sitarajii kusikia Kikwete akisema ataendelea na kipindi cha pili.
Tetesi za kusema kuwa yeye ataondoka baada ya kipindi kimoja zitatimia hata kama sababu nyingine zinavumishwa ni kuhusu hali yake kiafya.
Swali ni jee, Wapiganaji wanajiandaa vipi kujibu hili? na nani kati yao yupo tayari kugombea kumpinga Kikwete hata kama Lowassa hatachukua fomu?
kwani mkulu anasumbuliwa na nini jamani? mpaka hata waje wavumishe kwamba afya yake siyo nzuri.
Kikwete anaumwa, hapa kuna mambo ya privacy za ugonjwa, wanasema si ngoma lakini somewhat equally serious.
Kikwete anaumwa, hapa kuna mambo ya privacy za ugonjwa, wanasema si ngoma lakini somewhat equally serious.
Kwamba naiamini ama siiamini hii habari, ni mjadala mrefu na mpana maana sijui chanzo chake halisi cha aliyeiandika. Jambo la msingi ambalo ninaweza kuwa nakubaliana nalo ni kwamba EL anautaka URAIS, ni lini na kwa njia gani hilo nalo sijui.
Kwamba Lowassa hawezi kuwa Rais wa Tanzania, nalo siwezi kupingana na wewe ama kukubaliana nawe moja kwa moja maana nao ni mjadala mrefu sana kwa mazingira yetu ya sasa. Kuna vigezo vingi vya kuangaliwa na vyote vinaweza kuwa vya kufikirika maana lolote linaweza kutokea.
Kuhusu habari hii kuandaliwa na wanaompinga Lowassa, hilo naweza kupinga japo si kwa asilimia 100. Nina sababu nzito ambazo baadhi ya wahusika watakubaliana na mimi, na zaidi waandishi wa habari wenye kujua vyumba vya habari vya Tanzania vinavyoendeshwa ikiwamo Tanzania Daima Jumapili. Ni mjadala mrefu na mpana tupeane nafasi tusiubane.