The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252
Kuna njia kuu mbili ambazo kampuni/biashara huweza kuzitumia katika kutekeleza mkakati wake wa kiushindani (Competititve Strategy) katika soko; njia hizi hujumuisha;
- Offensive tactic; hii hutumika kipindi ambacho unaingia kwenye soko ambalo lina mwenyeji tayari (having established company/business).
- Defensive tactic; hii hutumika kipindi ambacho wewe kama kampuni/biashara umeshaingia sokoni hivyo unajihami juu ya kuingia kwa mshindani (new entrant) kwenye soko lako.
- Frontal assault; hapa huwa tunasema unafanya "head to head attacking" kwa maana ya kwamba utachofanya hapa ni kuiga kuanzia bei (price) mpaka mfumo wa usambazaji (distribution channel) anaotumia mtangulizi/mshindani wako. Njia hii ni ngumu kidogo, kwanza inakutaka uwe na rasilimali za kutosha, kwa sababu kufanya hivi huenda kukapelekea kumuamsha mshindani wako (awakening a sleeping giant) na akaamua kuchuana nawe vikali, kama hujajipanga vizuri kirasilimali, uwezekano wa kuondoshwa sokoni ni mkubwa.
- Flanking maneuver; Tofauti na kujilinganisha kwa kila kitu na mshindani wako; hapa utapaswa kuangalia eneo ambalo mshindani wako hafanyi vizuri (weak point), baada ya kung'amua hilo, jitahidi kwa upande wako kuwa mbora zaidi katika eneo hilo; kwa mfano huduma kwa wateja, mazingira ya biashara yako n.k
- Bypass attack; tofauti na kutumia njia tulizoona hapo juu; hapa unakuja kufanya kile kiitwacho "changing the rules of the game" kwa maana ya kwamba unakuja na bidhaa ambazo zitawafanya wateja waone bidhaa za mshindani/mtangulizi wako hazina umuhimu na ulazima (unnecessary). Kwa mfano kitendo cha Apple Company kuleta sokoni Ipod, kumefanya Sony Walkman kuonekana hazina umuhimu sokoni.
- Encirclement; tofauti na njia ambazo tumekwishaziona hapo juu, hapa utapaswa kuja na aina mbali mbali za bidhaa, zinazoanzia bei ya chini mpaka ya juu pia zenye kuhudumia kiasi kikubwa cha soko tofauti na kiasi cha bidhaa anachouza mshindani wako
- Guerrilla warfare; hapa utapaswa kufanya kile tukiitacho "hit and run" kwa maana ya kwamba utatumia njia tuliokwisha kuiona hapo mwanzo ya frontal assault ILA KWA KIASI KIDOGO SANA , intermittent assault. Hutopata faida kubwa sana, ila uzuri wa njia hii ni kwamba hutomfanya mtangulizi wako katika biashara ashtuke na aanze ku-deal nawe aggressively.
- Lower the inducement for attack; hapa utachopaswa kufanya ni kushusha bei ya bidhaa/huduma, kitendo hiki kitamfanya atakaye kuingia sokoni aone kwamba hakuna faida kubwa, hivyo hatovutiwa na soko, njia hii kwa kiasi kikubwa hutumiwa na Southwest Airlines ya U.S
- Raise structural barriers; hapa utachofanya ni kutoa kile kiitwacho "full line of products" kitendo hichi kwa kiasi kikubwa kitazuia au kupunguza ushindani. Miongoni mwa watumiaji wa njia hii kwa hapa Tanzania ni BAKHRESA GROUP (Azam) , hususani katika "Food and Beverage Business", hapa wamewezakuja na "range" tofauti tofauti za bidhaa kama vile maji, bidhaa za maziwa, vinywaji, juisi n.k
Ahsanteni
The Consult; +255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania
Kwa huduma za;
- Uandishi wa michanganuo ya miradi na mipango mkakati (Project Proposals &Strategic Plans)
- Utoaji wa semina na ushauri wa kitaalamu katika Usimamiaji wa miradi na Mipango Mkakati (Project Management & Strategic Management)
Your Success is My Desire