Mbinu ya kutokomeza uchawa kwa wana CCM na watanzania wengine

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
963
Reaction score
2,198
Kwa mtu anayefuatilia mambo ya nchi hii na anayejali mustakabali wa maendeleo ya nchi anajua kabisa uchawa kwa siku za hivi karibuni umeshusha uwajibikaji na hivyo unaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa kuliangamiza Taifa.

Zifuatazo ni mbinu zinazoweza kutumika kutokomeza tabia za uchawa japo kwa kiasi kikubwa mbinu hizi zinategemea wanaofanyiwa huo uchawa:-

1. Ikatazwe tabia ya kutaja taja majina ya viongozi au watu maarufu kwa kuyarudia rudia mara kwa mara. Kwa mfano; machawa wengi utawasikia

"namshukuru sana Mh. Rais, Dr., Mama Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania". Huku ni kupoteza muda na kuwachosha wasikilizaji/wasomaji

Kwani haitoshi kusema "...namshukuru sana Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania" bila kutaja jina lake? Nani asiyejua jina la Rais? Lengo la kutaja jina la mtu ni kumtambulisha kwa wasiomfahamu.

2. Viongozi wa Taasisi mbalimbali wawafundishe vijana kujiamini na kuthamini talanta zao. Unapomsifia mtu mwingine kupitiliza ndivyo unavyojishusha wewe. Unaonekana hauna unaloliweza zaidi ya kumtegemea unayemsifia

Unaweza kuongeza za kwako
 
nonsense article of the day, :1Head:
 
Uchawa ni kipimo cha akili. Hakuna mtu mwenye akili nzuri ambaye anaweza kuwa chawa. Uchawa unafanywa na watu ama wenye akili ndogo au ujuzi mdogo au wasio na weledi kabisa, wakiamini kuwa wanaweza kuziba mapengo yao ya akili, ujuzi na weledi, kwa kusifia watawala ili wawaone, kwa sababu utendaji, maarifa na akili haviwezi kuwashawishi watawala. Ukiona tu mtu ni chawa, ni dhahiri huyo ana kasoro nyingi, kuanzia upungufu wa akili, maarifa na weledi.
 
Katika wale maadui wa wakuu wa maendeleo waliotajwa na Hayati Nyerere, kwa sasa inabidi tuongeze na uchawa:
UJINGA
MARADHI
UMASKINI
UCHAWA
Nakazia ✍️
Machawa sio wazalendo, ni maadui wakubwa wa taifa. Imagine wanasifia kila jambo, hata wizi, ufisadi, utekaji, ufiraji, mauaji, nk !

Machawa ni janga la taifa, inafaa watambulishwe na kunyongwa hadharani ili kukomesha huo uovu

Lucas Mwashambwa Tlaatlaah ChoiceVariable stakehigh KERATO MOMBAA
 
Lakini tuwe tunaenda kulia lia mahakamani kwa haini maudenda?

1. Wanapomtaja taja rais samia huwa wanakuomba mdomo au hewa au pumzi au damu?

2. Wakimtaja wewe unapungukiwa nini?
Tuonyeshe unavyoathirika?
 
nonsense article of the day, :1Head:
Uchawa unadumaza, uchawa unashusha heshima, uchawa unamfanya mwanaume aonekane sho**uchawa unamfanya mwenye akili aonekane hamnazo

Hebu fikiria dume zima linasimama mbele za watu na kujibinua binua midomo kutaja taja majina ya watu na vyeo vya uongo na kweli kwa mbwembwe na kutafuta sifa za huyo mtu hata kama hazipo. Wewe unamchukuliaje?
 
jikite kwanye hoja biala kuweweseka gentleman,

hakuna haja ya mihemko nonsense kwenye mjadala :1Head:
 
Lakini tuwe tunaenda kulia lia mahakamani kwa haini maudenda?

1. Wanapomtaja taja rais samia huwa wanakuomba mdomo au hewa au pumzi au damu?

2. Wakimtaja wewe unapungukiwa nini?
Tuonyeshe unavyoathirika?
Tatizo la uchawa ndio limetufikisha kwenye hii hatua ya kufikiri. Yaani mtu akimkosoa mwingine anayefanya ushenzi kama huo uchawa anahusishwa na upande mwingine. Hizi ndio dalili za kukukosa akili na kumiliki akili za chawa

Tunafahamu akili za chawa zinaweza kumsaidia kukaa sehemu yenye uchafu ili apate chakula. Sasa mtu anayejiita chawa anawezaje kuwa na akili timamu?
 
Yes,
ni kweli kabisa tena una kera sana hasa kwa mamaluki malofa wa kibaraka wa mabwenyenye ya magharibi,

infact hiyo ndio asili yake :1Head:
Unaona sasa akili za chawa? Wote tunafahamu akili ya chawa inamuwezesha kuona chakula sehemu yenye uchafu tu, sasa binadamu anayejisifia kuwa chawa kama wewe anawezaje kuwa na akili timamu?
 
tuliza mihemko basi ndugu muerevu na mamaluki lofa wa kibaraka wa mabwenyenye ya magharibi,

usikose tena siku nyingine kubebwa ufala wa kifikra ili hatimae mkalipue vituo vua mafuta kana kwamba hiyo ndio haki yenu, sawa lofa?

uwahi ili upewe zawadi yako ya huzuni upeleke kwenye familia yaka, sawa muerefu lofa? :1Head:
 
Ulofa unadhihirika kupitia unachoandika. Hivi ukiwa unaandika maneno kama haya hujiskii vibaya? Hujionei aibu? Nafsi haikusuti? Sema ukweli
 
maisha magumu wale wapenda kitonga wamekimbilia fursa ya uchawa. Hawa kina mwashambwa, tlaatlaah,choice variable uvivu wa kufanya kazi wakaamua kuuza utu wao
 
Back
Top Bottom