MBINU KUU NNE (4) ZA KUONGEZA UBUNIFU KATIKA KAZI NA MAISHA

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,554
MBINU KUU NNE (4) ZA KUONGEZA UBUNIFU KATIKA KAZI NA MAISHA

“Pale ubunifu unapochangamana na utendaji wa bidii,ufanisi huchanua”

Kutokana na uchunguzi ulofanywa na jarida la Upreners wa mwaka 2018 umeonesha kua asilimia 68% ya watu wengi katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, hujihisi kuwa katika hali shinikizo [kutokuwa na utulivu wa kiakili na Amani] kiasi cha kutokuwa na ufanisi wala ubunifu katika kazi zao na kuishia kufanya kazi nyingi zisizo katika ubora tarajiwa.

“Pale ubunifu unapochangamana na utendaji wa bidii, ufanisi huchanua. Ndani ya Upreners tunategemea sana mawazo ya kila mfanyakazi wetu na uwezo wao wa kuyabadilisha mawazo yale yaweze kutoa suluhisho ambalo litaletea utoaji bora wa huduma zetu kwa wateja wetu lakini pia kuboresha mazingira yetu ya kufanyia kazi baina yetu Upreners Team” Mwisho wa kunukuu.

Zifuatazo ni njia kila mtu haswa viongozi waweza zitumia kuongeza ubunifu binafsi na wa wale wanaofanya nao kazi;

1.Tengeneza mazingira na mbinu ya kufanyia kazi mawazo yako ya kibunifu na yale ya wale unaofanya nao kazi.

Kuwa na mawazo ya kibunifu ni jambo jema lakini kuishia kuwa na mawazo ya kibunifu ni kazi bure, ni lazima kazi ya ziada ifanyike ya kutengeneza mazingira kwa ajili ya kuanza kufanyia kazi hayo mawazo ya kibunifu yaliyopatikana, unapokua umefanya uchunguzi yakinifu juu ya uwezekano wa kufanikiwa na kiutendaji wa wazo bunifu ni muhimu sana kuamua kuanza kuwekeza muda na rasirimali katika kuanza kulitendea kazi wazo hilo la kibunifu. Pale watu unaofanya nao kazi wanaona mawazo yao ya kibunifu yanafanyiwa kazi itawapa hamasa zaidi ya kuzidi kuwa wabunifu zaidi na hii huchipua ufanisi katika kazi.

2. Fanya maamuzi kwa kushirikishana na kuulizana na si kuamrishana

Watu wengi walio wabunifu hawapendi kuamrishwa sana, hupenda kufanya vitu kufuatia kusudio na kwa ridhaa ya mioyo yao. Na katika mazingira ya kazi hii lazima ianze kuwa tabia ya viongozi haswa wa juu na kama kiongozi ni muhimu sana kuwahamasisha uwaongozao kujenga tabia ya kutokuamrishana; bali kuelekezana majukumu kwa njia ya kistaarabu isiyo mfanya mwingine kujihisi kunyima uhuru wa kuchagua na kuamua na waonapo wewe kiongozi wa juu unaishi kwa utaratibu; hiyo mpya hata wao watavutika kuishi hivyo hivyo na hata kupelekea ubunifu kuongezeka na hivyo ufanisi kupatikana.

3. Jenga misingi ya kuaminiana na kuheshimiana baina ya viongozi wakubwa na wafanyakazi wa kawaida.

Mawazo bora ya kibunifu huweza tokea kutoka kwa mtu yeyote pasipo kuzingatia hali yake, elimu yake na cheo chake. Hivyo ni muhimu misingi ya kuheshimiana na kuaminiana ikajengeka ili kuruhusu wafanyakazi wote kuwa huru kuelezea mawazo yao katika hali ya kujiamini mbele ya watu wote na kuyafanyia kazi yote pasipo ubaguzi kwani hii itachangia ushirikiano na kujenga hali ya kujiamini na kujaribu zaidi hata kuchipua uwezo wa kibunifu ndani ya wafanyakazi wote, na hii huleta ufanisi katika kazi.

4. Futa tamaduni ya kushindikana kwa mawazo

Watu wengi sana ubunifu wa mawazo yao umepotea hivi hivi kutokana na hali ya kujiaminisha kuwa mawazo yao hayawezekani kwa sababu wanazoziita zipo nje ya uwezo wao. Hivyo ile hofu ya kushindikana kwa mawazo kumepelekea kuua uwezo wa kibunifu wa watu wengi, na hii inadhihirika katika kuogopa maneno ya watu wengine ikiwemo kebehi, dharau na vicheko. Na njia pekee ya kuiondoa hii tamaduni ni kuwajengea wafanyakazi wako uhakika wa kufaulu kwa mawazo yao na kuhakikisha wote wanaelewa mchango wa mawazo katika kufaulu kwenye jambo lolote.

Kushindwa ni moja ya njia muhimu sana kuanzisha na kuendesha biashara yeyote na kila kushindwa huleta mafunzo muhimu sana ambayo huchangia kuongeza ufanisi katika kazi. Tengeneza mazingira ambayo mawazo yaliyoletwa hayatazungumziwa katika vikao vya thathmini vya kikazi ama kuhuishwa katika utoaji wa fidia na kuishi na tamaduni kuwa njia pekee ya kua mbunifu zaidi ni kushindwa zaidi na kutafuta namna ya kuboresha utendaji wa pale paliposhindikana kwani hata watu wabunifu sana hukosea mara nyingi tu.

Nikutakie kila la kheri katika ubunifu wako wa kuleta mafanikio.

Kwakheri 2018 – Karibu 2019.
 
Back
Top Bottom