Mbeya: TANESCO yazima umeme Kiwira, Ofisi za Polisi

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Shirika la Umeme Tanzania Tanesco mkoani hapa, limesitisha huduma za umeme katika mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira (Kiwira Coal mine) na Ofisi za jeshi la polisi mkoani hapa baada ya taasisi hizo kushindwa kulipa madeni yanayodaiwa na shirika hilo.

Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mbeya, Benedict Bahati amesema mgodi wa Kiwira unadaiwa shilingi bilioni 1.3 na jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya linadaiwa shilingi milioni 700.

Bahati amesema wamefikia hatua hiyo kwa sababu wadaiwa hao hawajaonyesha nia ya kulipa madeni yao ambayo ni ya muda mrefu na hivyo kulisababishia shirika hilo kushindwa kujiendesha kwa ufanisi.


"Taasisi za Serikali ambazo madeni yake ni makubwa na mwitikio wake wa ulipaji sio mzuri, tumesitisha huduma mpaka watakapolipa madeni hayo", amesema.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashati amekiri kudaiwa deni na Tanesco pamoja na kusitishiwa huduma hiyo kwenye baadhi ya vitengo na kwamba wao kama taasisi wanadaiwa kama ilivyo kwa taasisi nyingine.

Mapema Mei mwaka huu, Rais John Magufuli aliiagiza Tanesco kuyakatia umeme mashirika na taasisi zinazodaiwa na shirika hilo.

Chanzo: Mwananchi
 
Hela ya bill ya umeme hapo polisi mbeya muulizeni yule aliyetwa kua kamanda wa kanda maalum ya DAR ambaye kwasasa ameshastaafu naamini atatusaidia
 
Hii ''kaaaaa-taaaa'' ni shida sana na ina ripple effect za kutosha. Unakatia umeme say mamlaka ya maji, wanashindwa kupump & kusupply maji, wananchi maskini wanaresort kwenye unprotected water ponds, wanaugua Kipindupindu, wanaenda kulazwa hospitalini na mwisho wa siku Serikali inawatibu bure kabisa - kwa gharama kubwa.

Japo dawa ya deni ni kulipa, nadhani TANESCO/Serikali ingetafuta njia nyingine bora zaidi ya kudeal na hawa wadaiwa sugu.
 
Walipe. Wahusika watumbuliwe.
Watumbukiwe vipi wakati fedha zinazoizinishwa na bunge. Hazina haizipeleki!! Walipe kutoka mifukoni mwao!! Hivi wakati CAG anasema pesa haziendi kama zilivyopitishwa hukumuelewa?? Wizara ipitishiwe labda 3bilioni, hadi sasa wamepewa bilioni moja tu!! Utegemee nini??! Yaani yeye atafute sifa wakati hatimizi majukumu yake, ili wengine waonekana hawafai sio uongozi mzuri.
 
Daah I know well the place nimesomea na nikawahi kufanya kazi hapo miaka kadhaa huko nyuma. Mgodi wenyewe umekwisha ule wanakatiwa na umeme tena naona ndo wanazidi kuichimbia zaidi futi6 ardhini.
 
Back
Top Bottom