Mbeya: Serikali kugharamia mazishi ya Alen Achiles aliyefariki baada ya kutoka Polisi

Mtu anaendesha maisha yake kwa taabu lakini jeshi letu dhalimu linaona hata maisha yale ya kuishi kama shetani, nayo hastahili.

Mungu mwenye huruma tunaomba uipokee roho ya kiumbe chako kinyonge. Kisasi kina wewe Bwana wetu Muumba mbingu na nchi.

Mungu wetu ututazame waja wako kwa jicho la huruma maana shetani yu milangoni mwetu kila siku akitumia pesa zetu kutesa, kuteka na kuwatengenezea kesi waja wako ambao uliwaumba wakiwa huru.

Bwana wetu hata tukulilie kwa sauti na machozi ya namna gani ili balaa linalotuzunguka lipate kutoweka?

Tegemeo la wanyobge wako ni wewe Bwana wetu uliyeweza kumwangusha hata Goliati kwa jiwe la mtumishi wako dhaifu, Daudi. Bwana tunakuomba, tenda muujiza dhidi ya wadhalimu wote.
 
it is like saying ,we will kill your loved one ,foot all burial costs and you do nothing but shed some tears which is free,the rest will be taken care of!
 
Siombi mambo haya yanitokee kamwe, ila kwa jinsi inavoendelea Hao wanafamilia walitakiwa wasipokee chochote na huyo aliyetoa hiyo ofa waombolezaji wangeanza naye Papo hapo.
NA HAKIKA TUTADAI PESA ZETU 26,042,018/=
WANANCHI TUACHE UOGA
 
Wanachi wengi mnapenda kusingizia polisi sababu wengi wenu ni wahaalifu kama c muhalifu Leo basi kesho utakuwa na wazo la kiharifu tu ndo maana mkiona sababu ya kulahumu polisi mnafanya justification mapema sana
 
Kwa hiyo kazi yao siku hizi ni KUTUUA NA KUGHARAMIA MAZIKO YETU ?

EWE MTAKA KUONGOZA MALAIKA WA MUNGU,umeamua kutumia kodi zetu kwa namna hiyo?.
e8667999930da7a7f66c3e4595a86583.jpeg
 
Wamesema kuwa yatagharamiwa? Kwanini iwapo alikuwa mtuhumiwa au hakuwa mtuhumiwa? Sijalipata vizuri hili
 
Wakati mwingne MAGUFULI mnamuonea tu....kama ambavyo mleta maada amekuja na kumhusisha RAIS as if ni yeye ndio kawatuma hao Askari
 
Hamna mchawi atuulie huyu MTU Maana Mungu yuko slow sana!! Jamani
Watu wa Dizain hii hawafi ng'o!
Tena waivi anaishi miaka mingi,Lazima aje ateseke kwanza ndo afe,
Maana damu za watu wote wale wanaouliwa lazima ifanye kazi vizuri ndipo afe.
 
Hapo hakuna cha uchunguzi wala nini. Walio ua wameua na wataendelea kutamba mitaani. Serikali nayo ishatoa laki mbili. Full stop. Maisha ya Allen ni kama ya mbwa hayakua na thamani.
 
Magufuli na serikali yako muunde tume ichunguze kifo cha huyo kijana,kuna maaskari wako responsible na hiki kifo,soi mugharamie mazishi then case closed,tunaongelea UHAI wa mtu umepotezwa kijinga,hao askari waliosababisha kifo watolewe hapo kituoni,hawafai nafasi ya u askari
 
Ungumbaru wa kumpiga mtu mateke/magongo ya mbavuni/tumboni - bila kujua kwamba kwa kufanya hivyo ni rahisi kumpasua mtu organ za ndani na kumuua! Polisi wapewe elimu mwafaka ili watu tuwe salama mikononi mwao!
Daaaah! Umeongea ukweli mkuu, tunapaswa kuwa salama tukiwa mikononi mwa polisi ili haki itendeke tukiwa salama na ukweli ujulikane.
 
Back
Top Bottom