Mbeya: Mtoto aliyezikwa jana akutwa chumbani kwake mara baada ya mazishi

Mlendamboga

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
665
338
Wakazi wa eneo la Isanga katika jiji la Mbeya wameendelea kushuhudia visa na mikasa, ushilawadu na matukio ya vioja, baada ya mtoto wa miaka 9 aliyekuwa amezikwa jana kwenye makaburi ya Isanga kukutwa akiwa kitandani kwake amelala usingizi mara baada ya kurejea kutoka makaburini.

Mara baada ya kufika nyumbani familia ikiwa inaingia ndani mwao, walipigwa na butwaa baada ya kukuta mtoto wao amelala kitandani kwake, na baada ya kuitana na kumwamsha mtoto huyo aliamka na kuonekana akishangaa hali aliyoiona pale nyumbani.
Kwa pamoja wananchi na wanafamilia walikubaliana asubuhi hii kwenda kufukua kaburi hilo ili waone nini kilichozikwa, na hivi dakika hizi zoezi hilo linaendelea na picha za makabuni hapo . MTAJUZWA KINACHOENDELEA

UPDATES KUTOKA ENEO LA TUKIO
KABURI LIMEFUKULIWA, HAKUNA KILICHOKUTWA NDANI YA KABURI YAANI MAITI ILIYOZIKWA JANA HAIMO!! POLISI WAMELAZIMIKA KUPIGA MABOMU ILI KUTAWANYA WATU PALE MAKABURINI BAADA YA KUANZA HALI YA SINTOFAHAMU JUU YA NINI KIMETOKEA?

KUTOKA NYUMBANI KWA FAMILIA KUFUATIA FAMILIA KUTOA MAELEZO YASIYOJITOSHEREZA JUU YA KUSAHAU MWILI WA MTOTO WAO, WANAKIJIJI AMBAKO BABA WA MTOTO NA FAMILIA YAKE ALIKUWA AKIISHI WAMEMTAKA MFIWA AHAME MTAANI MWAO KWAKUWA WANAMHISI ANAHUSIKA NA MICHEZO ILIYOTOKEA.

IMG-20170117-WA0060.jpg
FB_IMG_1484638858828.jpg

======

UPDATES:

Kutoka katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM wamemuhoji Kamanda wa Polisi wa Jiji la Mbeya ambaye amatoa maelezo kuwa, ushahidi wa kimazingira unaonyesha kuwa mwili wa mtoto huyo ulisahaulika kuwekwa katika sanduku na baada ya ibada mwili haukuagwa (Familia iliomba hivyo na ni kawaida).

Baada ya kuzika waliporudi nyumbani ndipo waliukuta mwili wa mtoto huyo ukiwa umelala kitandani. Jeshi la Polisi liliimarisha ulinzi katika maeneo hayo ya msiba.

Mmoja ya watangazaji wa Leo Tena amesema kuwa amewasiliana na mmoja ya wadau wake huko Mbeya na amemthibitishia kuwa kaburi limefukuliwa na jeneza limekutwa likiwa tupu halina kitu.

Inavyoonekana kuna uzembe katika kuandaa mwili na kuuweka katika jeneza, ingawa pia majirani na watu wanaoishi mazingira hayo wanahusisha na imani za kishirikina.

Tukio la mtoto wa miaka 9, Harun Kyando mkazi wa jijini Mbeya aliyefariki dunia jana na kuzikwa na baadaye kudaiwa kukutwa ndani nyumba, hatimaye amezikwa tena leo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo,Emanuel Lukula amethibitisha.
 
Wakazi wa eneo la Isanga katika jiji la Mbeya wameendelea kushuhudia visa na mikasa, ushilawadu na matukio ya vioja, baada ya mtoto wa miaka 9 aliyekuwa amezikwa jana kwenye makaburi ya Isanga kukutwa akiwa kitandani kwake amelala usingizi mara baada ya kurejea kutoka makaburini.

Mara baada ya kufika nyumbani familia ikiwa inaingia ndani mwao, walipigwa na butwaa baada ya kukuta mtoto wao amelala kitandani kwake, na baada ya kuitana na kumwamsha mtoto huyo aliamka na kuonekana akishangaa hali aliyoiona pale nyumbani.
Kwa pamoja wananchi na wanafamilia walikubaliana asubuhi hii kwenda kufukua kaburi hilo ili waone nini kilichozikwa, na hivi dakika hizi zoezi hilo linaendelea na picha za makabuni hapo . MTAJUZWA KINACHOENDELEA
Duuuuuu shikamoo [HASHTAG]#Mbeya[/HASHTAG] na maajabu yake
 
Mbeya washirikina sana
 
Aaaargh me siwez nikaamini hilo swala inawezekana kyna mistake zimefanyika mtu hamuwez kumzika af mkamkuta ety kalala ukifa bhn we umekufa tuu
 
Back
Top Bottom