Mbeya: Mama amchana mtoto kichwani kwa kumpiga na kuni kisa kuiba Tsh. 1,000, Mtoto ashonwa nyuzi

Mwanongwa

Senior Member
Feb 15, 2023
169
198
Mtoto Kuni.jpg
Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa Kata ya Ilemi, Mtaa wa Manga Veta anayejulikana kwa jina la Joshua Sanga amejeruhiwa kwa kupasuliwa kichwani, mtuhumiwa akiwa ni mama yake mzazi, ambaye inadaiwa alifanya tukio hilo baada ya mtoto kuiba kiasi cha shilingi elfu moja.

Joshua ambaye anasoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Veta, inadaiwa alitumwa na mzazi wake huyo kwenda kununua viazi, baada ya kurudi akaambiwa na mama yake kuwa ameiba shilingi elfu moja ambayo ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kununua kuni.

Mama huyo anayejulikana kwa jina la Tumaini John Seme ambaye pia ni mjumbe wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Kata ya Ilemi baada ya kuona pesa yake hajaiona ndipo akaanza kumpiga mtoto huyo kwa ukuni.

Kutokana na majeraha hayo mtoto Joshua ameshonwa nyuzi 3.

Taarifa ambazo zimepatikana mtaani hapo ni kwamba Tumaini Seme amekuwa na tabia ya kuwafanyia ukatili watoto wake pamoja na baba yao.

Uongozi wa Shule ya Msingi Veta baada ya kuona mwanafunzi ana majeraha wakamwandikia barua mama huyo lakini alikaidi na hakufika shuleni, Serikali ya Mtaa wa Manga Veta ikampa wito napo akakaidi.

SERIKALI YA MTAA KUMCHUKULIA HATUA
Mwenyekiti wa Mtaa Manga Veta, mina Mwenesi amesema “Hilo tukio ni la ukweli, mama hajakamatwa, tunaendelea kufanya mipango, Mganga Mfawidhi hakuwepo wakati wa tukio, baada ya hapo mchakato mwingine utaendelea.

“Tumeshamuita mara kadhaa lakini hafiki, huyo mama ni mjamzito na inadaiwa amekuwa na tabia ya kumshambulia huyo mtoto, hilo tukio la sasa ni mara ya tatu kuripitiwa.

“Amewahi kumchoma na mkasi na mtoto ana alama, hata kama mama mtu ni mjamzito, lakini anachokifanya si sahihi, tunataka kumchukulia hatua ikiwezekana akae ndani kwa muda ili ajifunze.

“Awali tulimuita kwa nia nzuri ya kuzungumza naye lakini amekuwa mgumu kutoa ushirikiano.”
 
Swala la wizi lishasahaulika, linaangaliwa jeraha!!

Malezi ya siku hizi yamekuwa magumu sana, unakuta huyo mtoto keshaonywa mpaka wazazi wamechoka. Kinachofuata ndiyo hicho sasa!!

Moshi, miaka hiyo tulikuwa na jamaa alikuwa dokozi sana tangu primary alipofika secondary akawa maradufu.

Wazazi waliongea wakachoka, siku hiyo baba yake alikamata akafunga kwenye mti akimninginiza kichwa chini mijuu guu!! Alipiga, alimchanja sana na kutia chumvi na pilipili then bakora sana.

Toka hapo jamaa aliacha wizi na kusimamia mosomo kwa bidii leo hii Boss mkubwa sana, anasema wazi kama si kile kipigo leo angeshachomwa moto na walimwengu!!

I'm sure kipigo kile leo hii yule baba angeonekana katili sana, hafai kwenye jamii!
So, huyo mama alipaswa amnunulie mtoto pizza na soda, ambembeleze mtoto aache wizi!!
 
Ni sawa ila kuna maeneo ya kupiga mtoto unapomwadhibu. Sio kichwani,tumboni,shingoni na maeneo mengine sensitive.ukinpa kilema ni wako bado utahangaika nae mwenyewe.so adhibu kwa akili.

Utapigaje na kuni kichwani? Akipasuka mishipa kwenye ubongo akavilia damu akafa?
Akipata ukiziwi ama upofu ama mtindio.
 
Mi nashangaa Sana
Ata biblia imeruhusu mapigo
 
Kwahio undhani kisa ni Buku ?

Kwa logic yako angeiba milioni moja ingebidi apigwe risasi ?

Tuache kuchukulia mambo kwa jumla jumla; hapo huenda issue ni bahati mbaya (hakutegemea atamuumiza hivyo sababu kisa ingekuwa buku na yeye anapenda pesa matibabu ni zaidi ya buku)

Hapo issue huenda ikawa ni tabia ya wizi ni mbaya (no matter unadokoa ngapi) au hasira na stress za mzazi kupelekea kufanya maamuzi ambayo anayajutia... All in all everycase should be looked at differently..., kwa huyu kuumia tusiseme kwamba watoto wasiguswe..., huenda hapa anakunjwa angali mbichi asije akachomwa moto na wananzengo kwa tabia yake chafu..., au akiwa Kiongozi akawa zaidi ya hawa wadokozi walamba asali....

Logikos Previous Known as KeyserSoze....
 
"Taarifa ambazo zimepatikana mtaani hapo nikwamba Tumaini Seme amekuwa na tabia ya kuwafanyia ukatili watoto wake pamoja na Baba yao."

Hapo hakuna cha bahati mbaya maana taarifa inasema huyo bimkubwa amekua na hio tabia ya kuwatembezea Ukuni mara kwa mara watoto pamoja na baba yao kila wanapozingua.
Kikubwa tumuombe bi Tumaini Seme apunguze ukatili kwa baba na watoto.
 
Ila taarifa inasema huyo bimkubwa amekua na hio tabia ya kuwatembezea Ukuni mara kwa mara watoto pamoja na baba yao kila wanapozingua.
Kikubwa tumuombe bi Tumaini Seme apunguze ukatili kwa baba na watoto.
Na tuwaombe pia baba na watoto.waache kuzingua...
Huyo mwizi wa rejareja akikua akakomaa wizini atatengenezwa jambazi wa baadae ambaye akikamatwa atapigwa na silaha nzito kuliko huo ukuni
 
"Taarifa ambazo zimepatikana mtaani hapo nikwamba Tumaini Seme amekuwa na tabia ya kuwafanyia ukatili watoto wake pamoja na Baba yao."

Hapo hakuna cha bahati mbaya maana taarifa inasema huyo bimkubwa amekua na hio tabia ya kuwatembezea Ukuni mara kwa mara watoto pamoja na baba yao kila wanapozingua.
Kikubwa tumuombe bi Tumaini Seme apunguze ukatili kwa baba na watoto.
Ukatili ni nini ? Unajua haya mambo ya after the fact mara nyingi yachukue with a pinch of salt....

Kuna mtu katika nyumba ya kupanga aliacha maji baada ya kufua ili yale maji baadae yatumike kwenda kumwaga chooni; bahati mbaya mtoto katika kucheza cheza kwake akadumbukia humo zikatokea complications baadae akafariki (Je ni Uzembe ?, Absolutely, ila je ni wangapi wanaacha ndoo au hata visima bila kufunika ?) Au watoto wanacheza bila uangalizi ?

Tukija kwenye hii case huenda huyu mama ana stress zake na ni mtu wa hasira, which is bad kwa mzazi ila haiondolei wajibu wa mtoto kuacha wizi, au tuamue kuwapangia wazazi wanaoona kufunza ni kwa viboko (spare the rod, spoil the child) Nina uhakika katika hizo hekaheka za mtoto ku-dodge hasira na upuuzi wa mzazi ndio mafunzo yenyewe hayo (hata ukubwani na maishani kuna vitu ambavyo atatakiwa kuvi-dodge Sisemi mama yupo sahihi (am neither a judge nor jury) lakini nachosema hizi blanket judgements ambazo zimefika mpaka mashuleni waalimu wamefungwa mikono kwa kutoa adhabu ni political correctness gone mad....
 
Ni sawa ila kuna maeneo ya kupiga mtoto unapomwadhibu. Sio kichwani,tumboni,shingoni na maeneo mengine sensitive.ukinpa kilema ni wako bado utahangaika nae mwenyewe.so adhibu kwa akili.

Utapigaje na kuni kichwani? Akipasuka mishipa kwenye ubongo akavilia damu akafa?
Akipata ukiziwi ama upofu ama mtindio.

Hakuna mzazi anataka kuumiza mwanae hivyo! Hata hicho kiboko unaweza ukamchapa takoni akaingiza mkono ukamvunja kidole au hata ukavunja mkono pia au akajirusha akajiangusha kwenye kuni kaumia kichwani! Tusemeje hapo??

Hapo mkifuata kiundani vizuri! Hiyo unaweza kukuta ni ajali pengine alikuwa anarukaruka! Ama mtoto alitaka kujibizana (kupigana) na mzazi, mzazi akapandwa hasira akatumia silaha iliyopo au mtoto mwingine maneno machafu huku anakimbia, tupia ukuni huyo akafie mbele!!

Hayo yote watu hawayaoni, wanachoona ni jeraha la mtoto!! Kuna mitoto nunda kwelikweli, jamii yote inakusema wewe!! Achana na malezi kabisa mrembo
 
Inawezekan ni bahati(mbaya au nzuri).
Najaribu tu kuwaza ingekuwa fimbo ya mwalimu ndo imechana kiganja tu achilia mbali kichwa...
 
Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa Kata ya Ilemi mtaa wa Manga veta anayejulikana kwa jina la Joshua Sanga amepasuliwa kichwani na mama yake mzazi akituhumiwa kuiba kiasi cha shilingi elfu moja.

Joshua ambaye anasoma darasa la sita katika shule ya msingi Veta ,inadaiwa kuwa alitumwa na mama yake kwenda kununua viazi na baada ya kurudi akaambiwa na mama yake kuwa ameiba shilingi elfu moja ambayo ilikuwa ni maalumu kwaajili ya kununua kuni.

Mama huyo anayejulikana kwa jina la Tumaini John Seme ambaye pia ni mjumbe wa jumuiya ya wazazi CCM kata ya Ilemi baada ya kuona pesa yake hajaiona ndipo akaanza kumpiga mtoto wake na ukuni.

Kutokana na majeraha hayo mtoto Joshua ameshonwa nyuzi 3 na pia Joshua amedai kuwa hii siyo Mara yake ya kwanza kwa mama huyo kumpiga na ukuni.

Taarifa ambazo zimepatikana mtaani hapo nikwamba Tumaini Seme amekuwa na tabia ya kuwafanyia ukatili watoto wake pamoja na Baba yao.

Uongozi wa shule ya msingi veta baada ya kuona mwanafunzi Joshua anamajeraha wakamwandikia barua mama huyo lakini alikaidi na hakufika shuleni, na serikali ya mtaa wa Manga veta nao ukamwita kwenye kikao napo alikaidi.

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
Wewe ni Nani kuingilia malezi ya mtoto asiyekuhusu ambae anafunzwa na mama yake?
Huo upuuzi ndio unasababisha mitoto yenu haina maadili mazuri.
 
Swala la wizi lishasahaulika, linaangaliwa jeraha!!

Malezi ya siku hizi yamekuwa magumu sana, unakuta huyo mtoto keshaonywa mpaka wazazi wamechoka. Kinachofuata ndiyo hicho sasa!!

Moshi, miaka hiyo tulikuwa na jamaa alikuwa dokozi sana tangu primary alipofika secondary akawa maradufu.

Wazazi waliongea wakachoka, siku hiyo baba yake alikamata akafunga kwenye mti akimninginiza kichwa chini mijuu guu!! Alipiga, alimchanja sana na kutia chumvi na pilipili then bakora sana.

Toka hapo jamaa aliacha wizi na kusimamia mosomo kwa bidii leo hii Boss mkubwa sana, anasema wazi kama si kile kipigo leo angeshachomwa moto na walimwengu!!

I'm sure kipigo kile leo hii yule baba angeonekana katili sana, hafai kwenye jamii!
So, huyo mama alipaswa amnunulie mtoto pizza na soda, ambembeleze mtoto aache wizi!!
Mkuu,kizazi hiki ni kibovu sana na hao wanaounga mkono wizi wa huyo mtoto,siku akiwa jambazi watawageukia wazazi kuwa wamelea mtoto wao vibaya.
 
Hakuna mzazi anataka kuumiza mwanae hivyo! Hata hicho kiboko unaweza ukamchapa takoni akaingiza mkono ukamvunja kidole au hata ukavunja mkono pia au akajirusha akajiangusha kwenye kuni kaumia kichwani! Tusemeje hapo??

Hapo mkifuata kiundani vizuri! Hiyo unaweza kukuta ni ajali pengine alikuwa anarukaruka! Ama mtoto alitaka kujibizana (kupigana) na mzazi, mzazi akapandwa hasira akatumia silaha iliyopo au mtoto mwingine maneno machafu huku anakimbia, tupia ukuni huyo akafie mbele!!

Hayo yote watu hawayaoni, wanachoona ni jeraha la mtoto!! Kuna mitoto nunda kwelikweli, jamii yote inakusema wewe!! Achana na malezi kabisa mrembo
Nakuunga mkono.
 
Back
Top Bottom