Kuna watu wenye juhudi sana ktk kazi lakini kuna watu wenye juhudi kuzidi wengine.
Wakati wafanyakazi wengine wakiibia serikali hasa muda wa kazi na hata kufanya mambo yao mengine wakati wanapaswa kufanya kazi ya umma.
Hali ni tofauti sana kwa Mwalimu Anael Kiwale wa shule ya msingi Mwanyanje jijini Mbeya kata ya Igawilo Uyole njia panda.
Huyu mwalimu kwa kweli ni anayeweza kujihimu asubuhi saa kumi na mbili akawahi shuleni akaandaa mazingira ya kufundisha wanafunzi wake na saa moja kasoro akawa na wanafunzi darasani na hata akiombwa na wanafunzi ambao pengine hawakuelewa darasani wakati wa kawaida wa masomo haoni hatari kuwasadia mpaka waelewe.
Kizuri zaidi hufanya yote haya bila kudai malipo yoyote japo ikitokea mzazi mwenye uelewa kiasi anaweza kumpa lift hata njiani kwa kutambua juhudi yake.
Nimejikuta nikiandika hapa baada ya mwanangu aliyefika darasa la nne akiwa hajui kusoma wala kuandika lakini nilipomkabidhi mikononi mwake miaka minne iliyopita mpaka sasa amefaulu darasa la 7 matokeo ya 2017.
Inasemekana hana digrii kama wengine lakini kwa juhudi ni zaidi ya maprofesa.
NINGEKUWA MHUSIKA NINGEMPANDISHA DARAJA.Mwisho samahani kwa nitakao kuwa nimewakwaza kwa kuandika haya ila niseme waalimu wote igeni juhudi hii.
Jamii na Mungu tunaona mnachofanya wengine mnadhamini hela kuliko utu.
Wengine wako radhi kuuza maandazi muda wa kazi kwenu niseme kama ualimu haulipi ila kuuza maandazi kunalipa kwanini? msiache kazi ya ualimuu mkauza hayo maandazi mjue kuna watu wako mitaani miaka mitano sasa wanatamani ajira zenu hizo hawazipati wanaomba kila kukicha Mungu amewasikia sijajua atawajibu lini?
HONGERA SANA KIWALE MWALIMU WANGU WA MWANYANJE.