Mbeya City yatimuliwa uwanja wa Sokoine

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Meneja wa Uwanja wa Sokoine wa jijini hapa, Modetus Mwaluka ameitaka Mbeya City itafute uwanja wake wa kufanyia mazoezi badala ya kuugeuza uwanja huo kuwa wa mazoezi.

Mwaluka alitoa agizo hilo jana alipozungumza na mwandishi wa gazeti hili kuhusu sababu za kuizuia timu hiyo kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Sokoine unaomilikiwa na chama tawala, CCM.

“Uwanja huu ni wa mashindano na siyo wa mazoezi kwani mazoezi ya kila siku yanaharibu uzuri ya uwanja.’’

Mwaluka alisema kwa kawaida Uwanja wa Sokoine unatakiwa kutumika siku mbili na timu mbili zinazotarajiwa kumenyana.
Msemaji wa Mbeya City, Dismass Ten alipoulizwa alisema ni kweli waliambiwa kuhusu suala hilo na kwamba wanachofanya kwa sasa ni kutafuta viwanja vingine.

‘’Mbeya City ni timu ya halmashauri inayomiliki viwanja vingi vya shule, hivyo ni suala la kocha kuangalia kiwanja kizuri ambacho kitatumika kwa mazoezi’’ alisema.

Kwa kipindi kirefu, timu hiyo imekuwa ikijinasibu kwamba itamiliki uwanja wake eneo la Iwambi, lakini mpaka sasa hakuna dalili za kutengeneza uwanja huo.

Source:Mwananchi
 
Back
Top Bottom