Mbeya City yachanja mbuga

Mbeya City yachanja mbuga

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,154
Reaction score
64,491
Dar es Salaam. Mbeya City imetinga robo fainali ya michuano ya Nile Basin inayoendelea nchini Sudan baada ya kutoka suluhu na Enticelles ya Rwanda juzi usiku katika Uwanja wa Khartoum, Sudan.


Kutokana na matokeo hayo, Mbeya City sasa itaikabili Victoria University ya Uganda kesho katika Uwanja wa Khartoum, katika robo fainali ya michuano hiyo mipya iliyo chini ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).


Timu hiyo ambayo ilimaliza Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa katika nafasi ya tatu imeshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza na imecheza mechi tatu, imeshinda moja, imefungwa moja na sare moja.


Mbeya City iliyokuwa katika Kundi B imemaliza hatua ya makundi ikishika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi nne ikitanguliwa na AFC Leopards ya Kenya inayoongoza kundi hilo kwa kuwa na pointi tisa.


Enticelles imeshika nafasi ya tatu kwa pointi mbili na Academie Tchite ya Burudi imemaliza mkiani mwa Kundi B kwa pointi moja iliyovuna sare na timu ya Rwanda.


Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi, aliliambia gazeti hili kuwa wanashukuru kufika robo fainali kwani michuano ni migumu lakini wanaendelea kupambana licha ya uzoefu mdogo wa michuano ya kimataifa walionao.


“Tumekuja kushindana na si kushiriki, lengo letu tufike fainali na tubebe kombe, tutapambana hadi hatua ya mwisho na tunaomba Mungu atusaidie malengo yetu yatimie,” alisema Mwambusi.


Mechi nyingine zitakazochezwa kesho ni kati ya wenyeji El Ahli Shandi dhidi ya Malakia ya Sudan Kusini, AFC Leopards ya Kenya itaikabili Defence ya Ethiopia kabla ya wenyeji Al Merreikh kuumana na Academie Tchite ya Burundi.


Michuano hii imeanzishwa kwa mara ya kwanza na Cecafa kwa ajili ya mabingwa wa nchi ama timu zilizoshika nafasi ya pili.


Chanzo:Mwananchi
 
mwananchi kwa nini walikuwa hatangazi tangu mwanzo

Kila la Heri Mbeya City !
 
Hongereni Mbeya City, watanzania tupo nyuma yenu
 
Back
Top Bottom