mujungu
Senior Member
- Nov 1, 2010
- 143
- 55
Limeanza kuwa jambo la kawaida kusikia Chadema na CCM wamepigana, damu imemwagika ,wameenda polisi nk. Wengine wanasema hata bila woga chama fulani kinataka watoto wenu wafe, wambieni wasikifuate. Chama fulani ni chama cha kigaidi,Muuaji ni nani?gaidi anayejulikana kwanini asikamatwe? Kwa hii mbegu iliyopandwa tutavuna mazao yake? Kwani angalau hata bangi ulimwa kifichoni,lakini hii inapandwa adharani kwa baraka zote za Wazee .kisha tunawekewa matangazo kwenye redio na tv mimi fulani bin fulani meneja mkubwa sana tuienzi amani ya Tanzania isipotee. Hivi tunamaanisha au tunaigiza? Utabiri mwingine ni rahisi kama hekaya za abunuasi na mkata tawi alolikalia.
Badala ya kusikia hoja za wagombea kwenye huu uchaguzi ,kila uchapo ni matukio ya fujo. Hivi mazao ya hii mbegu yanavunika? Tusimame tuisaidie Tanzania kwa moyo wa dhati, kwani mbegu inakua kwa kasi ya ajabu.