Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Leo Mbatia ambae ni waziri kivuli wa wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano akiwa anasoma hotuba ya kambi ya upinzani bungeni pamoja na mambo mengine ameongelea suala la utumbuaji majipu linalofanyika chini ya awamu ya tano.
Mbatia ameongelea sakata la uuzaji nyumba za serikali lililofanyika kati ya mwaka 2002 na 2004 kwa nyumba zaidi ya elfu saba na kuitaka serikali ya awamu ya tano izirejeshe nyumba hizo mara moja kama azimio lililopitishwa na bunge lilivyotaka kwa kuunga mkono agizo la Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kurejesha nyumba hizo kwa serikali kwa ambazo ziliuzwa kinyume cha utaratibu ikiwemo kuuziwa kwa wasioukuwa watumishi wa umma na zile ambazo hazikupaswa kuuzwa kama zilizopo kwenye maeneo ya utawala wa serikali.
Mbatia alisema wanajua uuzaji wa nyumba hizo ulisimamiwa na waziri ambae ndie Rais wa sasa hivyo atekeleze ili waone usafi wake katika jamii.
Kuhusu kivuko cha Bagamoyo, Mbatia amesema kivuko hicho ni jipu ambalo limeiva kwa viwango vyote vya sasa na linatakiwa litumbuliwe mara moja. Mbatia amesema ni wazi kivuko hiko kilichonunuliwa na TEMESA chini ya usimamizi wa waziri wa ujenzi wa awamu ya nne ambae ndie Rais wetu wa sasa kwa mujibu wa ripoti mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali alibaini ununuzi wa boti feki na mbovu na kugharibu dola za kimarekani milioni nne nukta tisa. Mbatia alihoji alipo tabibu wa kutumbua jipu hilo.