Mbatia kutimuliwa UKAWA?

Status
Not open for further replies.
Mbatia mtumishi wa serikali hata lipumba pia ni mtumishi wa serikali hangaikeni mtarudia round about.

Kwani mbatia hapo kawekwa na nani.? Lipumba umnamuonaje.? Na slaaa nae eti na kadi ya ccm vp.? Ccm ina wataaalam kwel kwel....!
 
Hahahaha, hatudanganyiki, sisi ukawa ni mbele kwa mbele

Mbona mlisha danganyika mkasusia bunge.? Kwenye msafara wa mamba na kenge wamo....sema nia yenu ilikuwa njema lkn mlizidiwa tu kdg.
 

Mshindwe na mlegee...mbinu chafu za ccm,hizi.
Nani kawaambia ukawa kuna shida hiyo zaidi ya kupigana na CCM?
 
Siku moja ukweli ukijulikana uliopo ndani ya chadema kuhusu mabele malando na mwesigwa baregu hamtaamini wote hao ni watumishi wa serikali ukawa zungukeni sana baada ya uchaguzi mkuu ndiyo mtayajua haya wakati huo mtakuwa peupe kama karanga.

watumishi wa serikali ndo wazuri wakiwepo kwani wataongeza ujuzi ktk serikali ya ukawa.
 
Siku moja ukweli ukijulikana uliopo ndani ya chadema kuhusu mabele malando na mwesigwa baregu hamtaamini wote hao ni watumishi wa serikali ukawa zungukeni sana baada ya uchaguzi mkuu ndiyo mtayajua haya wakati huo mtakuwa peupe kama karanga.

Hizo ni njama tu za CCM, kwani ni wapi hakuna matatizo. Leo hii kamati ya maadili ya CCM inaketi kufanya kitu gani kama huko kuko shwali. Tatizo linalowatafuna ni Urais kila moja na lake. Sasa kama CCM chama kikongwe kuliko vyote bara la Afrika senior members wanapalaganyika hadi kamati ya maadili inakaa kuwajadili unashangaa nini tatizo kama hili hilo likitokea UKAWA. Majibu yenu ni Oktona mwaka huu na wala si mbali, tuone kama hata katika uchaguzi mkuu mtawaapisha hata walioshindwa kwenye uchaguzi. UKAWA ina wasomi wengi na wazuri haiwezekani kila kitu wakakubaliana bila hata kupingana (zidumu fikira za mwenyekiti na wote bila haya wakasema zidumu) hiyo haitakuwa demokrasia tuynayoitaka.
 
Mpinzani wa kweli atatoka CCM.Hivi chuo cha magogoni bado kinafundisha propaganda?
 
Nilitaka kuandika kitu kinacho fanana na maandiko yako, cause umeisha andika niishie tu kukupongeza that you are the great thinker.
 
Tafuteni kazi nyingine ya kufanya hii haina tena mashiko wala faida.
Hamchoki kujipigia ngoma na kucheza wenyewe?
Hiyo ngoma vipofu tu ndio wanaweza kuicheza, wengi wanaona hawachezi ng'oo imekula kwenu.
 
kwani wewe inakuathiri nini ukawa ikisambaratika na wewe ni ccm mm ninathani ungefurahia tu...hivyo ondoka sasa moja kwa moja mpaka limumba wakupe ujira wako mkuu.
 
Hawa ni waandishi wa gazeti gani? Hivi kuna mtu anaweza kweli kwa mazingira yasiyokuwepo katika bunge la katiba uwepo wa ukawa ungekamilika maamuzi tofauti na ilivyotokea?
 

Kuna taarifa za upotoshaji zinasambazwa kwa nia ya kuwachanganya wananchi kuhusu Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na viongozi wake wakuu.

Ni wazi taarifa hizo zinasambazwa na 'wale wale' ambao hali yao ya kisiasa iko mtanzikoni na hatma yao ya kubaki madarakani iko hatarini, kadri UKAWA unavyozidi kuimarika na viongozi wakuu wa umoja huu wakizidi kushirikiana kwa dhati kuwaonesha Watanzania njia sahihi ya kufikia mabadiliko ya kweli ya kimfumo na kiutawala, kwa kuiondoa CCM madarakani.

Hofu ya watawala kutokana na uimara wa UKAWA ni kubwa. Uoga wa kushindwa uchaguzi wa mwaka huu umezidi kuwakumba tangu baada ya anguko kubwa walilopata kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Hawana tena hoja za kushawishi. Kutunga uongo kama huo wa 'Dkt. Slaa na James Mbatia', ndiyo kete zao zilizobakia.

Imani na matumaini ya Watanzania kwa UKAWA na viongozi wake ni kubwa mno. Kila mara viongozi wa UKAWA wanaposikika wamekutana kujadili masuala makubwa ya kitaifa kwa maslahi ya wananchi, watawala wanaweweseka.

Taarifa za upotoshaji eti kwamba hakuna maelewano kati ya Katibu Mkuu wa Makatibu Wakuu wa UKAWA, Dk. Slaa na Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA James Mbatia, si uongo wa kwanza wa 'watawala waliojawa uoga'. Wamejaribu mara kadhaa. Hawajafanikiwa. Hawataweza. Kwa sababu UKAWA ni tumaini la watu.

Waliojawa uoga kwa sababu ya uimara wa UKAWA, wamejaribu mara kadhaa kutunga maneno ambayo wanadhani yanaweza kuwakatisha moyo. Ni wale wale ambao huko nyuma walieneza chuki ndani ya jamii kwa kusema chama fulani cha dini fulani, kabila fulani, kanda fulani. Kote huko wameshindwa. Wanabuni ugomvi usiokuwepo wala usiotarajiwa kuwepo.

UKAWA unasonga mbele. Ndilo tumaini la Watanzania. Maelewano miongoni mwa viongozi wote wakuu yanazidi kuongozwa kwa dhamira na nia safi ya kuwaongoza wananchi kupigania matamanio ya haki na matumaini waliyonayo.

Badala ya kuzubaishwa na uzushi wa 'ugomvi' miongoni mwa viongozi wa UKAWA, unaoratibiwa na makanika wa uongo walioko madarakani, Watanzania waendelee kusimama bega kwa bega na viongozi wa UKAWA kuendelea kushusha tumaini hili la Watanzania nchi nzima na kuzidi kuchochea moto wa mabadiliko unaokwenda kuwachoma watawala, Oktoba, mwaka huu.

Ni hayo kwa sasa.

Makene




 
Mkuu
Asante sana kwa taarifa sahihi.

Maccm ndiyo yanazidi kuchanganyikiwa wakisikia hii kitu.

Tuna imani sana na Mbatia, Tuna imani kubwa na Prof. Lipumba tunaiman kubwa sana Dr. Slaa na UKAWA.
 
Tulianza na Mungu, tutamaliza na Mungu.

Watashindana lakini hawatashinda.

Wao na pesa za ufisadi, dhuluma na vitisho vya dola, sisi na Mungu na wazalendo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…