Mbakaji ahukumiwa viboko 20 Nkasi

Mbakaji ahukumiwa viboko 20 Nkasi

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

LAW1.jpg

IJUMAA, SEPTEMBA 19 2014

MKAZI wa Kijiji cha Karundi, Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa, Moses Kang'ombe (17), amehukumiwa adhabu ya kuchapwa viboko 20 baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji na kusababisha mimba.

Hukumu hiyo imetolewa juzi na Mahakama ya Wilaya hiyo baada ya kumtia hatiani katika makosa mawili la ubakaji na kusababisha mbakwaji ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba (jina tunalihifadhi), kupata mimba na kushindwa kufanya mtihani wa kuhitimu mwaka huu.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ramadhani Rugemalila, alisema mshtakiwa alikiri kosa hivyo Mahakama ilimtia hatiani chini ya kifungu cha 130 (1) na (2)( e) na 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.

Alisema katika kosa la kubaka, atachapwa viboko 12 na kosa la kumpa mimba mwanafunzi huyo, atachapwa viboko vinane.
Awali Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Hamimu Gwelo, aliiambia mahakama hiyo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo mwaka huu na baada ya mwanafunzi huyo kukutwa na mimba.

Aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa mshtakiwa iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ya kuwabaka wanafunzi na kuwasababishia mimba. Mahakama ilitoa adhabu hiyo kwa kuzingatia umri wa mshtakiwa mwenye miaka chini ya 18.

CHANZO: Majira
 
Naona ametumia umri wake kuepuka adhabu, hii sheria inahitaji review kwa watu wa 14-17
 
Viboko vinne kwa ajili ya mimba? Hiyo ndio adhabu kali aliyopewa mbakaji? kweli mahakimu na mahakama pamoja na sheria zipo na zinafanyakazi.
 
Viboko vinne kwa ajili ya mimba? Hiyo ndio adhabu kali aliyopewa mbakaji? kweli mahakimu na mahakama pamoja na sheria zipo na zinafanyakazi.

jifunze kusoma kabla hujakurupuka, kwanza huyo aliyedaiwa kubaka ni mtoto yuko under 18 na pili issue ya kubakwa imechomekewa tu huyo dogo ni mtu na demu wake tu sema ndo ivyo bado mdogo na yuko lasaba!!!
 
Nawe usikuruuke kuandika/kujadili vitu usivyovijua. Nakupa home work: Tafuta ingredients za kubaka? FYI: unaweza kashitakiwa kwa kosa la kumbaka hata mke wako!
 
kama ni hivyo siangechapwa tu humo staff room yakaishia shuleni,.afu baada ya adhabu ya hivyo viboko20 jamaa anakuwa huru?mbona katoto atakoma coz anakatoto tumboni dah majanga
 
Nilitegemea kuwa angepelekwa gereza la watoto
 
Kwa kawaida kuna jela za watoto ndo ilitakiwa apelekwe. huyu mbakaji atakua ni mtoto wa kiongozi wa ccm kama kawaida yao
 
jifunze kusoma kabla hujakurupuka, kwanza huyo aliyedaiwa kubaka ni mtoto yuko under 18 na pili issue ya kubakwa imechomekewa tu huyo dogo ni mtu na demu wake tu sema ndo ivyo bado mdogo na yuko lasaba!!!

Inaelekea una matatizo ya akili kijana, unajua kosa la kubaka? hata mkeo wa ndoa au gf kama unamuingilia bila ya ridhaa yake au kumlazimisha inakuwa kama umembaka. Kama angekuwa ndio mwanao au dada yako kabakwa ungesema hivyo? Hebu jifunze kufikiria kabla ya majibu ya kukurupuka kama umetoka lumumba.

Kwa hiyo kama ni demu wake basi anahaki ya kumbaka? Usitulete akili za kiccm hapa
 
Nina Mashaka na uwezi wako. A cha kupotosha.
 
Back
Top Bottom