Mazuri ya CCM

kutafuta mazuri ya ccm ni km kutafuta mazuri kwa shetani,hata ukiyapata hakumfanyi kuwa kundi jema.
 
Salam wana jamvi,

Kwa muda mrefu humu jamvini tumekua tukishuhudia threads nyingi zilizojikita kwenye kutoa malalamiko au kukosoa upande wa pili.
Imefikia hatua sasa watu wamejikuta wakichangia mada kwa kuangalia nani ametuma hiyo post, na kama ni mtu wa upande wa pili basi yataanza kuporomoshwa matusi bila hata kusoma na kuelewa maudhui ya mtoa mada.

Kukosoana kwa nia ya kujenga sio kitu kibaya kwani kunamfanya mkosolewa kujirekebisha if at all he/she has positive attitude.

Nafikiri sasa tuangalie na kujikita pia kwenye kufichua mambo mazuri yanayofanywa na serikali (CCM) kwa upande mmoja na vyama vya upinzani (CDM) kwa upande wa pili.

Wafia chama wa ccm wajikite kueleza mazuri yao na upinzani wakosoe hayo mazuri kama wanahisi si mazuri kwa mustakabali wa nchi and the vice versa is true.

Ccm waeleze bayana wameifanyia nini nchi hii na wataifanyia nini nchi hii, vivyo hivyo vyama vya upinzani vieleze vimetimiza vipi majukumu yao kama vyama vya upinzani na vitafanya nini vitakapoingia madarakani.

Hizi habari za kila siku dr. Slaa, dhaifu, fastjet, mwigulu, nape, walibelali zingekupungua ili kuondoa mazingira ya kujenga taifa la walalamishi na vijana wenye chuki kwa viongozi wao.

Ukitabasamu unaongeza siku za kuishi, basi tupate mda wa kutabasamu kwa kusikia mazuri yanayotendeka nchini.
 



Mkuu naona kama unanitia uchungu na hasira tu ! si afdhali tusingekuwa na uhuru kuliko hao waliopigania uhuru wanachokifanya! mkoloni alikuwa anakusanya kodi kibabe lakini si alikuwa anatibu watu bure!Hilo LCCM unalodai linatoa elimu burehiyo bure linayotoa ina tofauti gani na gharama make mtoto akimaliza shule hajui kusoma na kunandika si gharama tu hizo. Hivi unajua gharama za kukaa na wajinga wasio jua kusoma na kuandika? KI UKWELI CCM HAKUNA JEMA HATA MOJA TUNALOWEZA KULIORODHESHA HAPA. Labda mseme maandiko tu! yapo mazuri ila watekelezaji sifuri
 
Huyu jamaa aneonesha dhahiri kuwa ccm ilikuwa ya zamani na sio sasa wakati ikiwa TANU,hapa hajaweka suala la maendeleo akijua wazi kuwa ccm haija fanya lolote..fisadi mkubwa wewe,andika basi na mabaya yake kwani hakuna mazuri pasipo na mabaya.
 
"wali...", "ili..." "wali..." ...tunataka useme "wana", "ina".
Hii hoja ni ngumu kwa maana hakuna chama kingine kimepata nafasi ya 'kuonyesha mabaya yake', labda tuilinganishe na TANU au mkoloni!
 
Ni kweli CCM ya akina Nyerere, Kawawa, Karume na wengineo walifanya hayo uliyoyasema. Hoja ni je, tuendelee kuishi kwa kutumia historia ya ccm, wakati ccm ya jekei, kinana, mwigulu na wengineo ilishabadili sera, itikadi na mwekeleo wake? Tafakari!!!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…