Wanajamvi nimeona leo tujadili mazuri ya CCM ambayo wameyafanya ili tuone upande mwingine wa shilingi maana hapa kila kitu kina pande mbili.
1. Uomoja kitaifa
2. Amani na Utulivu
3. Kuondoa udini
5. kuukema ukabila
6. Daraja la Kigamboni coming soon
7. kukubali upinzani
8. Ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wote ambapo collateral ni deposits zao za NSSF na PFPF PPF
9. Ujenzi wa babrara nchi nzima
10. Ujenzi wa Udom na vuo vikuu vingi vya kumwaga.
11. Misamaha ya kodi kwa wawekezaji kiasi cha TZS 2trilion kwa mwaka inayowawezesha kuendelea kuwepo na kutoa ajira kwa watz
12. Shule za kata nchi nzima maarufu kama vodafasta
13. Mikataba mizuri kwenye sekta ya madini inayoiwezesha serikali kukusanya mrabaha wa 3%
15. Mikataba mizuri ya mafuta na gesi inayotuwezesha kukusanya kodi tu lakini kukosa umiliki wa rasilimali hiyo muhimu
16. Mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura inayotuwezesha kupata umeme wa dharura japo kwa bei ya kifisadi.
17. Imewezesha kukua kwa sekta ya anga (Precision, Fly540, Zara, nk) japo shirika letu linadidimia/kufa.
18. Imewezesha uhusiano wetu na India kukua kwa kutumia vema hospitali zao kwa tiba za viongozi wetu.
19. Imewezesha viongozi wetu wengi kufanikiwa kumiliki nyumba maeneo nyeti kwa kuwauzia kwa bei poa.
20. Imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwaondoa wachimbaji wadogo maeneo yenye madini kwa lengo la kuwapatia wawekezaji wakubwa ambao watalipa mrahaba wa 3%
Kwa kweli mambo ni mengi ndugu Senkenke1 ukifanikiwa kuyataja yote ni nani asiye upande wetu atakayehimili kusimama na kusikilizwa?