simon mato
JF-Expert Member
- Sep 27, 2015
- 926
- 485
Ndugu wanajamvi,
Kama kawaida yetu sisi wanaharakati na wazalendo wa hii nchi kuweka mambo mazito katika taifa hili bila kujali itikadi zetu.Kuna mambo mengi yanamulikiwa na tochi katika utawala wa awamu ya tano na Mimi nimekaa chini na kutafakari na kuja na ujumbe kwenu JF na watanzania wote kuhusu utawala wa awamu ya tano.
TUANZE NA MAZURI YALIYOFANYWA KWENYE AWAMU YA TANO:
1: Kujenga serikali ya UWAJIBIKAJI NA UWAZI: hapa Rais amefanya kazi ngumu kweli kuhakikisha serikali yake inawajibika kwa wananchi bila kujali itikadi za ki vyama,kidini ,kikabila na kikanda. Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikiwajibika ipasavyo kwa wananchi kwa hili tumemshukuru sanaa Rais kwa kazi aliyoifanya.
2: Kuusambaratisha mtandao wa mafisadi; hapa Rais wetu alijitoa kafara kuhakikisha anapambana na huu mtandao hatari kwenye nchi yetu. Watumishi hewa zaidi ya elfu kumi waliokuwa wanakula kodi ya wananchi wamefukuzwa na wengine kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa kosa la kuhujumu uchumi.
Kwa kuwa siku zote Rushwa ni adui ya haki wananchi walikuwa wanateseka kupata Huduma za kijamii, hivyo MAGUFULI amefanya kazi nzito kuhakikisha kodi za wananchi inatumika ipasavyo hapa pia Tunamshukuru Rais wetu kwa dhati.
3: kujenga utawala bora; hapa tunachukilia mfano kwa kuwapa nafasi nyeti vijana wenye maono ya mbali katika kulipigania taifa hili kama POLEPOLE , MAKONDA,NAPE,MWIGHURU, UMMY,JAFFO,JANUARY na wengineo kwa kuwa vijana pia wana mtazamo pana kwenye dhana ya maendeleo hii imemsaidia sanaa RAIS kujenga utawala bora.
Pia ni Mara ya kwanza Tanzania katika awamu hii wasomi wengi wenye weledi wa hali ya juu wanapewa vyeo katika serikali, kama; prof. Mbarawa,prof.Ndalichako,prof.Muongo na wengineo wengi wenye hekima,busara na maarifa. Hii imemsaidia sanaa Rais kujenga serikali yenye Uzalendo wa hali ya juu na yenye maono ya mbali kuelekea kwenye uchumi wa kati.
3: Ujenzi wa demokrasia ya kweli; hapa ndipo kuna upotoshaji mwingi kuhusu hili dhana, lakini Mimi kwa maoni yangu pamoja na kufanya tafiti mbali mbali kwenye Jamii utawala wa MAGUFULI unafuata misingi ya katiba ya Jamhuri ya muungano. Wale wanaolalamika ni wale ambao hawajui misingi ya utawala bora na maana ya demokrasia.
Tunamsihi RAIS MAGUFULI aachane na magenge yenye mrengo wa kutugawa kwa kupotosha umma kuwa nchi haiendeshwi kwa kufuata katiba. Na ushauri wa bure ni kwamba wakitaka demokrasia ya kweli waanze kujitawala kwenye vyama vyao kwa kuzingatia katiba ya kweli kwa kuwa wameshindwa kuzuia ata migogoro ya kikatiba kwenye vyama vyao.
4: upatikanaji wa Huduma za kijamii kwa haraka na kwa ufanisi; sote tumeona wananchi wakishukuru mhe. RAIS MAGUFULI hadharani kwa kuhakikisha wananchi wanapata Huduma za kijamii kwa harakati na kwa ufanisi wa hali ya juu. Hosptalini na mashuleni kote huku Huduma imekuwa kwenye misingi ya haki yake.
MABAYA KWENYE HII AWAMU YA TANO:
kusema kweli Mimi kama mwananchi wa kawaida sijaona tatizo baya zaidi ya kujukwa kwenye genge la mabeberu ambao wanampotezea mda katika kuleta maendeleo kwa watanzania. Namsihi Rais wetu aachane mara moja na hili genge la kuunda mizengwe ya kila aina kwa kuwa wanaochelewa kupata maendeleo ni wananchi na siyo hawa watu.
Ogopa sanaa chama cha siasa kinachofanya siasa za matukio na miujiza, kwa kuwa wanatengeneza propaganda nyingi kwenye hizo matukio yenye mrengo wa kuchonganisha wananchi na utawala ni vyema hili genge likapuuzwa kabisa.
Chukulia mfano; hali ya maaafa kagera sote tunajua serikali ya kweli ni ile inayoratibu mambo yake kisayansi lakini wana propaganda hawalijui hili. Maafa ikitokea lazima serikali ichukue takwimu na kupanga namna ya kuwasaidia wananchi na hii lazima ichukue mda kwa sababu mambo haya ni ya kisayansi hayaitaji kukurupuka kama wao walivofikiria.
Kingine Rais hajaenda bukoba wameongea weee, wengine wakisema huyu ndiye anayejiita Rais wa wanyonge hastaili ata kidogo lakini ni mangapi Rais ameshirikiana na wananchi hadharani kwenye matukio mbali mbali ya kitaifa. Jibu ni nyepesi tuuh wao kwao Siasa ni matukio basi, hawana mikakati mizito ya kushauri serikali zaidi ya propaganda tuu.
Wanachokitafuta hasa ni nini kwa Rais wetu? Akitulia wanaongea na kuweka nongwa weeeee lakini akinguruma pia siku hiyo hawalali kumwekea kila aina ya mizengwe na kuanzisha naye vita ya kimtazamo kwenye utawala wake. Hili genge linalojisadifu kuwa wako karibu na wananchi wakati wa matukio tuwaogope vibaya mno.
Nitoe rai yangu kwa watanzania wote kuwa mabadiliko ya kweli tutayapata chini ya uongozi wa RAIS MAGUFULI na siyo wale waliyotaka kutuaminisha kuwa mabadiliko ni kuzungusha mikono kwa dakika tano. Ni vyema tukawapuuza kama tulivowapuuza kwenye sanduku la kura 2015.
Safari ya kuelekea uchumi wa kati bado inaendelea;
Ni wako kijana mtiifu, mzalendo na mwanaharakati wa kweli Tanzania.
SIMON MATO.