simon mato
JF-Expert Member
- Sep 27, 2015
- 926
- 484
- Thread starter
- #21
Uwe wa kwanza kuacha unafiki kwa kumkemea mwenyekiti wako wa chama aache ubabe na kuacha kuendesha chama kama Mali yake! Hapo utakuwa umesaidia sanaaa na utakuwa mzalendo wa hali ya juu kama mimiUzi wako ni wa hovyo kabisa, ni wa kujipendekeza! serikali hii imeonyesha ubaguzi mkubwa sana kwa kuwaajiri makada wa CCM tu kwenye nafasi za utendaji kama Ukurugenzi. Huu ni udhaifu mkubwa ambao haujawahi kutokea kwenye tawala zilizopita. Kwa upande wa Huduma za kijamii, mashuleni watoto wanakosa hata karatasi za kufanyia mitihani yao kisa elimu bure, tumeshuhudia kukosekana kwa chanjo muhimu sana katika hospitali zetu, sijui unafahamu matokeo ya kukosa chanjo wewe? Upande wa demokrasia kwa utawala huu umeiminya demokrasia kwa kiwango cha kutia aibu, hata mtoto mdogo anafahamu. Kifupi uache unafiki ili usaidie Taifa lako.