Mazungumzo ya Soko la Pamoja EAC yakwama

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Mazungumzo ya Soko la Pamoja EAC yakwama
Faraja Mgwabati
Daily News; Thursday,November 13, 2008 @21:15

Mazungumzo ya kuanzishwa kwa Soko la Pamoja la Afrika Mashariki yamekwama baada ya Tanzania kugomea baadhi ya vipengele ambavyo imeona vina maslahi kwa taifa. Mazungumzo hayo ambayo yanafanyika chini ya Jumuiya ya Afrika Mashiriki (EAC) ilibidi yakamilike mwezi ujao, lakini kutokana na kushindwa kufikiwa kwa mwafaka, yamesogezwa hadi Aprili mwakani.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala alisema Dar es Salaam kuwa Tanzania haijakubaliana na mawazo ya nchi nyingine kuhusu uhuru wa kusafiri, mgawanyo wa ardhi, uraia wa kudumu na masuala ya huduma. Dk. Kamala alisema baadhi ya nchi zinataka soko la pamoja likianzishwa, kuwe na uhuru na haki ya kupata ardhi, kitu ambacho Tanzania inakataa kwa sababu nchi nyingine haina ardhi ambayo Watanzania wataweza kupata.

Alisema pia sheria za ardhi za nchi hizo zinatofautiana, kitu kitakacholeta mtafaruku ambao mwisho wa siku, Tanzania ndiyo itaathirika kwa nchi nyingine kuchukua ardhi kwa kuwa ina ardhi kubwa. Tumeona suala la ardhi tusiliingize kabisa kwenye suala la soko la pamojaukitaka kuleta machafuko basi ingiza suala la ardhi kwenye soko la pamoja, alisema Dk. Kamala ambaye pamoja na Kamati ya kisekta ya Mawaziri wa EAC walikutana Zanzibar wiki hii.

Kuhusu uraia wa kudumu, Dk. Kamala alisema Tanzania inapinga kuwapo kwa haki ya kupata uraia kwa wananchi waliokaa ndani ya nchi moja kwa miaka mitano, kwa sababu itailazimisha Tanzania kuwapa uraia hata wageni ambao wamekaa nchini isivyo halali. Alisema Tanzania itaendelea na utaratibu wake uleule wa kuwapa uraia wageni wenye sifa ili kuziba mianya ya wachache ambao wanaweza kutumia mgongo wa soko la pamoja kukaa nchini.

Kamala alisema Tanzania pia inapinga mawazo ya baadhi ya nchi kutaka vitambulisho vya uraia vitumike mipakani badala ya pasipoti ili kurahisisha wasafiri kuingia nchi nyingine kwa urahisi. Alisema mazungumzo hayo yataendelea tena Machi mwakani na kama hadi Aprili mwafaka hautafikiwa, basi wataongeza muda zaidi, lakini Tanzania haitakubali kwenda haraka kama itaona hakuna manufaa.
 
Dk. Kamala alisema baadhi ya nchi zinataka soko la pamoja likianzishwa, kuwe na uhuru na haki ya kupata ardhi, kitu ambacho Tanzania inakataa kwa sababu nchi nyingine haina ardhi ambayo Watanzania wataweza kupata.

Tukubaliane tu kwenye maswala ya uchumi, biashara, currency etc, haya mengine naona ni kuingiliana kwenye mambo ya ndani, I strongly oppose this agenda! Nakubaliana na kupinga suala la ardhi. Suala la ardhi si la kucheza nalo.
 
Mara chache huwa wanaweka maslahi ya Watanzania mbele. Huu ni uamuzi ambao utaungwa mkono na Watanzania wengi. Hivi Burundi, Rwanda, Kenya na Uganda wana ardhi kweli iliyobaki kwa wanajumuiya wengine?
 
Kimsingi binafsi nakushukuru Mh. Kamara kwa msimamo wako juu ya swala hili la Ardhi na EAC. Pamoja na umuhimu wa EAC, tofauti zetu kiuchumi, kisiasa na kijamii hazipaswi kufumbiwa macho.

Kwa maoni yangu Mh. Kamara kama swala hili halitafikiwa muafaka endelevu April, itakuwa vema likiahirishwa kwa kipindi kisichopungua miaka 2 ili kila pande ikajadili kwa kina kabla ya kurudi mezani tena.

Watanzania wanamakovu mengi sana kutokana na majeraha yaliyotokana na wenyedhamana kutowajibika. Hebu wapeni muda kidogo watibu makovu haya kabla hamjawaongezea majeraha mengine.
 
Binafsi naunga mkono kwa serikali ya Dar kuwa na msimamo thabiti juu ya umiliki wa ardhi yetu, kuna maswala ambayo jumuia ingeyafanya kwa utaratibu wa kueleweka, Ningeonelea swala la matumizi ya sarafu moja ndo lingekuwa linaongelewa kwa kipindi hiki baada ya kumaliza mambo ya customs, Kuna wajanja wameliweka hili swala la sarafu nyuma kwa manufaa yao binafsi hivyo basi Dk. Diodorus Kamala lazima ukomae!!!!
 
Niliangalia TV wakati waziri Kamala akiongea nilijisikia vizuri kweli kweli. Kumbe kuna watu wanaweza simamia maslahi ya nchi vizuri namna hii kwenye serikali ya awamu ya nne!!! Swala la ardhi lisiletewe mzaha hata kidogo...hapo ndipo machafuko hutokea.

Kenya ardhi yao waliipoteza kwa walowezi na mafisadi wa serikali yao...wabaki tu huko huko.Najisikia vizuri kuwa Mtanzania..mmmh TzPride.

Waziri Kamala sisi tuko nyuma yako, weka maslahi ya nchi mbele na Mungu atakubariki.

Mungu ibariki Tanzania
 
Mazungumzo ya Soko la Pamoja EAC yakwama
Faraja Mgwabati
Daily News; Thursday,November 13, 2008 @21:15

Mazungumzo ya kuanzishwa kwa Soko la Pamoja la Afrika Mashariki yamekwama baada ya Tanzania kugomea baadhi ya vipengele ambavyo imeona vina maslahi kwa taifa. Mazungumzo hayo ambayo yanafanyika chini ya Jumuiya ya Afrika Mashiriki (EAC) ilibidi yakamilike mwezi ujao, lakini kutokana na kushindwa kufikiwa kwa mwafaka, yamesogezwa hadi Aprili mwakani.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala alisema Dar es Salaam kuwa Tanzania haijakubaliana na mawazo ya nchi nyingine kuhusu uhuru wa kusafiri, mgawanyo wa ardhi, uraia wa kudumu na masuala ya huduma. Dk. Kamala alisema baadhi ya nchi zinataka soko la pamoja likianzishwa, kuwe na uhuru na haki ya kupata ardhi, kitu ambacho Tanzania inakataa kwa sababu nchi nyingine haina ardhi ambayo Watanzania wataweza kupata.

Alisema pia sheria za ardhi za nchi hizo zinatofautiana, kitu kitakacholeta mtafaruku ambao mwisho wa siku, Tanzania ndiyo itaathirika kwa nchi nyingine kuchukua ardhi kwa kuwa ina ardhi kubwa. “Tumeona suala la ardhi tusiliingize kabisa kwenye suala la soko la pamoja…ukitaka kuleta machafuko basi ingiza suala la ardhi kwenye soko la pamoja,” alisema Dk. Kamala ambaye pamoja na Kamati ya kisekta ya Mawaziri wa EAC walikutana Zanzibar wiki hii.

Kuhusu uraia wa kudumu, Dk. Kamala alisema Tanzania inapinga kuwapo kwa haki ya kupata uraia kwa wananchi waliokaa ndani ya nchi moja kwa miaka mitano, kwa sababu itailazimisha Tanzania kuwapa uraia hata wageni ambao wamekaa nchini isivyo halali. Alisema Tanzania itaendelea na utaratibu wake uleule wa kuwapa uraia wageni wenye sifa ili kuziba mianya ya wachache ambao wanaweza kutumia mgongo wa soko la pamoja kukaa nchini.

Kamala alisema Tanzania pia inapinga mawazo ya baadhi ya nchi kutaka vitambulisho vya uraia vitumike mipakani badala ya pasipoti ili kurahisisha wasafiri kuingia nchi nyingine kwa urahisi. Alisema mazungumzo hayo yataendelea tena Machi mwakani na kama hadi Aprili mwafaka hautafikiwa, basi wataongeza muda zaidi, lakini Tanzania haitakubali kwenda haraka kama itaona hakuna manufaa.

....Hapa angalau serikali ya CCM ilitumia akili msimamo huu wenye maslahi kwa taifa ndio ulio sababisha leo wenzetu wa EAC watutenge....
 
Uzuri ea watanzania ndio huu kukitokea kiongozi wa CCM au serikali ya CCM ikaonyesha msimamo kwenye kulinda maslahi ya taifa lazima watatoa pongezi na kuunga mkono hoja bila kinyongo licha ya utofauti wa kiitikadi hebu cheki humu kwenye huu uzi kila mtu anamsapoti wazir kamara......
 
Back
Top Bottom