Mazungumzo na Mjengwa: Wasifu wa Julius Nyerere, Bi. Chiku bint Said Kisusa, kutoka jikoni hadi Mnazi Mmoja

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255
MAZUNGUMZO NA MAGGID MJENGWA WASIFU WA JULIUS NYERERE: MAMA SAKINA BI CHIKU BINT SAID KISUSA WANAWAKE KUTOKA UANI HADI UWANJANI MNAZI MMOJA KUDAI UHURU

Mara ya mwisho kumuona Mama Sakina, yaani Bi. Chiku Bint Said Kisusa ilikuwa katika miaka ya 1980 nimekaa barzani Saigon Mtaa wa Narung'ombe na Sikukuu na rafiki yangu marehemu Ashraka.

Asharaka akanigutua kunambia, ''Mohamed unamuona Mama Sakina huyo anapita?''

Naam ilikuwa ni yeye Bi. Chiku bint Said Kisusa, mke wa Shariff Attas kavaa baibui lake la ukaya anapita anavuta miguu.

Mama Sakina alikuwa kachoka kawa mtu mzima, mzee sana.

Kwangu mimi Mama Sakina ni bibi yangu na wanae Mwalimu Sakina na Mwalimu Fatna mimi ni shangazi zangu na kaka yao Mustafa, rafiki ya baba yangu yeye ni baba kwangu.

Hivi ndivyo tulivyofunzwa na wazee wetu na hii ndiyo ilijenga ule udugu uliokuwapo Dar es Salaam baina ya familia zetu.

Watoto wake hawa wawili wa kike Mwalimu Sakina, na Mwalima Fatna walikuwa walimu wakisomesha Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika Muslim School.

Mwalimu Sakina alikuwa bingwa wa Kiingereza ukimsikia anazungumza utafurahi.

Siku moja kulikuwa na khitma nyumbani kwake Mtaa wa Pemba basi tumekwenda.

Sisi watoto wa nyumbani baada ya kula barazani tunaingia uani ambako huwa ni sehemu ya wanawake.

Huwezi kutoka barazani ukaruka kizingiti ukenda uani kwa wanawake ila uwe mtoto wa nyumbani.

Khitma hii ilikuwa ya kumrehemu Abdallah Ibrahim mtoto wa Ibrahim Hamisi ndugu yake Mwalimu Sakina.

Ibrahim Hamisi ni mmoja wa waasisi wa African Association, 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 pamoja na Kleist Sykes.

Baba yake alikuja kutoka Dafur, Sudan mwishoni mwa miaka ya 1800 kama askari wa Kinubi wakati ule ule walipoingia akina Sykes kutoka Imhambane, Mozambique wote hawa wakiwa askari mamluki katika jeshi la Wajerumani kuja kupigana na Bushiri bin Salim Al Harith na Chief Mkwawa.

Nyumba ya Mzee Ibrahim Hamisi Mtaa wa Kipata na Congo haikuwa mbali na nyumba niliyozaliwa mimi, Mtaa Kipata na Swahili.

Baada ya shughuli rafika yangu marehemu Omar Sykes kanyanyuka twende tukamwamkie Mwalimu Sakina uani.

Mwalimu Sakina kakaa kwenye kiti kwani wakati huu alikuwa mtu mzima sana tena kavaa baibui lake la ukaya kazungukwa na akina mama wakubwa na wadogo wote wamekaa katika majamvi na mikeka.

Omar ni mtoto wa kaka yake kipenzi Abdul Sykes.

Ile hata Omar hajamfikia alipokuwa kakaa katikati ya watu ile kumtia machoni tu, Mwalimu Sakina akapiga ukelele,
''Omar how nice to see see you, tell me Omar have you eaten?''

(Omar nimefurahi kukuona wewe ushakula?)

Rafiki zetu na jamaa zetu ambao hawamjui Mwalimu Sakina walikuwa kama wamepigwa na radi kwani ile, ''intonation,'' na ''construction,'' ya lugha na kiliwashtua zaidi ni kuwa anaezungumza ni mama mzee wa Kiswahili tena yuko ndani ya baibui.

Baada ya kutoka pale ilinipata kazi kubwa ya kuwaeleza hawa jamaa zangu kutoka Oyster Bay, Masaki, Mbezi Beach na Mikocheni, Mwalimu Sakina ni nani.

Nikawaambia Mwalimu Nyerere mwenyewe alikuwa anatulia anabaki kutabasamu tu kila akisikia Mwalimu Sakina anavyommwagia Kizungu.

Nimeyaleta haya kwa kuwa kuna watu wengi hawajui historia ya wazee wetu wakati wanadai uhuru wakidhani kuwa zile baibui na kanzu zilikuwa ni kielelezo cha ujinga.

Sina haja ya hapa kueleza ilm ya dini waliyokuwanayo vichwani mwao na juzuu ngapi walikuwa wamehifadhi na kuweza kusoma ghibu yaani, ''off head.''

Hawa akina mama ndiyo Abdul Sykes aliowaleta katika mikutano ya TANU akimtumia Bi. Chiku bint Said Kisusa kuwakusanya ikawa mkutano ya mwanzo ya TANU ukiangalia picha unayaona mabaibui yalivyojaza uwanja.

Leo waliobakia ambao wanaweza wakahadithia siku hizi muhimu katika historia ya nchi yetu ni watu wachache sana.

Mimi nawajua walio hai watatu tu - Mama Maria Nyerere, Abbas Sykes na Bilal Rehani Waikela.

Picha ya kwanza kulia ni Maalim Sakina bint Arab, picha ya pili mwanamke pekee ni Mwalimu Sakina, kulia wa kwanza Ali Mwinyi Tambwe, Oscar Kambona, Ali Jumbe Kiro wa tano Julius Nyerere. Picha ya tatu wa kwanza ni Bi, Chiku bint Said Kisusa, Bi, Titi Mohamed, wa kwanza kulia Bi. Tatu bint Mzee Julius Nyerere huyo katikati safari ya kwanza UNO anasindikizwa Uwanja wa Ndege,1955.

MAALIM SAKINA.jpg

MWALIMU SAKINA, ALI JUMBE KIRO, ALI MWINYI TAMBWE NA JULIUS NYERERE.jpg

TATU BITI MZEE.JPG

 
Sijui kwa nini mmeshindwa kuwaenzi hao wapendwa wenu.
Laki...
Nadhani tuliamini kuwa kutunza kumbukumbu na historia ya nchi ni jukumu la serikali kwa hiyo hapakuwa na juhudi zozote za kufanya hilo.

Lakini ilipodhihirika kuwa zimeandikwa historia nyingi tu ila hii ya wazee wetu ndiyo hivi sasa tumeamua kuwaadhimisha wazalendo hawa sisi wenyewe nje wa utaratibu uliozoeleka na leo ndiyo hivi tuko hapa barzani tunawajadili.
 
Back
Top Bottom