Maziwa yanayofaa kwa mtoto mwenye umri wa siku 84

Lubengera

JF-Expert Member
Jun 21, 2019
822
1,305
Ndugu zangu wataalamu wa Afya, naomba ushauri juu ya maziwa yanayofaa kwa mtoto mwenye umri wa siku 84

Mke wangu amemaliza likizo ya uzazi, na hivyo kuanzia Jumatatu ataanza kuingia office, kipindi akiwa ofisini ni vyema mtoto kupewa maziwa.

Hivyo naombeni ushauri maziwa yanayofaa kwa mtoto ambaye umri wake ni siku 84 mpaka sasa.

Nitashukuru kwa msaada wa ushauri wenu
 
Mnunulie CMA no 1 haya ni kwa ajili ya infantry .

Infacare no 1 pia ni mazuri niliyanunua kwa ajili ya second born wangu alipozaliwa maziwa ya mama yalikuwa hayamtoshi.
 
Nashukuru sana kwa ushauri
 
SMA no.1 ni mazuri sana mkuu pia inabidi mkeo ayaandae mwenyewe ili anayekaa na mtoto aweze kumix kwa urahisi na ni vizuri kujua mtoto anakunywa mls ngapi maana unaweza andaa 240mls akatumia 150mls yanayobaki unamwaga kujua mls za mtoto itakusaidia sana.
 
inawezekana mama akishamaliza kumnyonyesha asubuhi anakamua maziwa yake na kuyaweka kwenye friji kisha anapewa mtoto baadaye na isitoshe kwa mama mwenye mtoto huwa anafanya kazi nusu siku kwa hiyo atawahi kumnyonyesha mtoto. Niliwahi kusikia uji mwepesi wa unga wa muhigo ni mzuri sana kwamtoto ila kama kuanzia miezi sita kama sijakosea (nadhani unaweza kufuatilia kujua muda halisi wa mtoto kunywa huu uji). Kuhusu aina ya maziwa unaweza kupata mazia mazuri ila mtayarishaji akashindwa kutayarisha katika hali ya usafi na kumpa mtoto kwa wakati muafaka
 
ni kweli mkuu lakini mara nyingi tunakamau kabla mtu hajarudi job unakuwa na stock ya kutosha kama mimi nilivyokuwa home nilikua napata mpaka 800mls kwa siku ila nilivyorudi job supply ilipungua hadi 400mls kwa siku uzuri ile stock ilinisaidia kutompa mtoto maziwa ya kopo. inabidi elimu itolewe kama mama anaweza kunyonyesha miezi 6 maziwa yake ni vizuri kwa wale wenye supply ya maziwa mengi.
uji ni mpaka miezi 6 japo kuna watu wanaanza kuwapa wakiwa na miezi 4 na usafi ni muhimu sana na chupa za mtoto inabidi zioshwe zenyewe na hazichanganywi na vyombo vingine.
 
Nadhani kigugumiz kinaanza hapo kwenye kuweka maziwa ya binaadamu kwenye fridge.wengi huchukulia kama uchafu.elimu elimu elimu bado.

Back
Top Bottom