Kama mama yupo mwambie amnyonyeshe. Kama hayupo, yanaeza kupewa mtoto hayo ya ng'ombe, lakini kuna jinsi ya kuyachanganya na maji ili mtoto aweze kuyadigest vizuri. Ukikosea mtoto ataugua sana.
If nakumbuka vizuri, kwa mfano unataka nusu lita, chukua nusu lita ya maziwa, ichemshe kwanza, then weka kando.
After hapo chukua nusu lita ya maji masafi chemsha na yenyewe weka kando.
Ukimaliza hapo changanya maji na hayo maziwa, approximately itakua kama lita nzima, chemsha tena kwa pamoja taratibu mpaka yapungue yafike nusu lita. Hapo ndo unapoza na kumpa mtoto yakiwa yamechanganywa.
Popote ulipo ukienda hospitali ya wilaya utakuta wale ma bibi lishe hua wanatoa maelekezo zaidi
Maziwa plain ya ng'ombe hua yana protein content kubwa sana ambayo tumbo la mtoto mdogo hua haliwezi kudigest. So ukiwa unampa yalivyo bila kuchanganywa hua anaanza kuharisha na sometimes anakua anapata kama allergic reactions.
So badala ya kumsaidia unakua unamuuguza na inaeza kusababisha mtoto kupata utapiamlo na pia kushindwa kukua sawasawa na umri wake, au even worse kifo.
I stand to be corrected.