Mambo ya dhuluma kwa wananchi nilikuwa nayasikia South Africa,Zimbwabwe,katika utoto wangu nilishiriki katika nyimbo za Kaburu kamata kamata,haini smith ,mchokozi Banda,sikutegemea katika maisha yangu haya mambo nitayaona katika nchi yangu nzuri ya Tanzania nilikozaliwa na ambako nitazikwa,kweli ni kichefuchefu,Askari wanapora maiti wanaenda kutupa barabarani,mbona tumeona Raisi Kikwete akiahirisha mkutano Namibia kuja kumzika Jini Lake,Sheikh Yahaya,hivi katika nchi hii kuna ambao wanavibali vya kuzikwa kama binadamu na wengine kutendwa kama wanyama,Polisi anayang'anya maiti kwenda kutupa barabarani mambo gani hayo mbona yanatisha
Uko wapi utawala wa sheria
Yuko wapi KIKWETE aliyesema maauaji hayatatokea tena mbele ya uso wake
Kweli tunaserikali
wanataka wananchi tuamua tutakayo ,sawa bwana bado kitambo kidogo amini usiamini nchi hii itarudi kwenye enzi zake